
_Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam _*Mh Paul Makonda*_ _leo tarehe 08/08/2017 (siku ya siku kuu ya nane nane) *saa nane mchana* atazungumza na wananchi wa *Bunju* na viunga vyote vya karibu katika soko la Bunju ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh Rais, *Dr John Pombe Magufuli* alilolitoa jana alipokutana na kusalimiana na wananchi wa maeneo hayo akitokea ziarani Mkoani Tanga._
_*Mh Mkuu wa Mkoa ataongozana na viongozi wote wa Mkoa na wilaya wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Salum Happi,Mstahiki Meya Mh Benjamin Sitta, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Diwani kata ya Bunju, wataalam wote kutoka idara mbalimbali za wilaya ya Kinondoni na Ofisi ya Mkoa.*_
_Hii ni fursa ya kipekee kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam hususani wakazi wa wilaya ya Kinondoni kujitokeza kwa wingi ili kutoa kero na changamoto zao na kupatiwa ufumbuzi yakinifu._
_Watu wote mnakaribishwa._
No comments:
Post a Comment