Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu (wa tatu
waliokaa), leo Agosti 20,2017 ameongoza uzinduzi wa albamu ya injili ya
mwimbaji Elineeema Babu (wa tatu kushoto) uliofanyika kwenye uwanja wa
Stendi Mpya ya Ikungi.
Katika
uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu ameendesha zoezi la uuzaji wa albamu hiyo
iitwayo TARATIBU NITAFIKA na kusaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi
Milioni Tatu ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.
Mhe.Mtaturu
amewahimiza waimbaji wa nyimbo za injili wilayani humo kutumia vyema
fursa waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha amani na upendo
nchini, akitolea mfano kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza iliyoimba
wimbo uitwao AMANI kwa ajili ya kuhamasisha amani nchini.
Mwimbaji
Elineema Babu ameachia albabu ya tatu iitwayo “Taratibu Nitafika” yenye
nyimbo nane ambapo amewasihi wadau wengine kumsaidia kwa kununua albamu
hiyo (Audio) ili aweze kupata shilingi Milioni Sita zinazohitaji ili
aweze kurekodi video ya albamu hiyo. Taratibu Nitafika ni albamu ya tatu
baada ya kutanguliwa na albamu mbili ambazo ni Nitumie pamoja na Fanya
Kazi ya Bwana.
Mwimbaji Elirehema Babu akitumbuiza kwenye uzinduzi huo hii leo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alikuwa mgeni rasmi
DC Ikungi akizindua albamu hiyo
DC Ikungi akionesha albamu iliyozinduliwa leo
Mkuu
wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD
Katibu wa CCM wilayani humo (kulia) kwenye uzinduzi wa albamu ya
mwimbaji Elineema Babu
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Baba Askofu wa Jimbo la Singida Dkt.Paul Samweli
BMG Habari
No comments:
Post a Comment