• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 20 August 2017

    Rais Shein alitema chehe baraza la mawazi Zanziba

    Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein amewataka mawaziri kuhudhuria Vikao na Ziara zake ili waweze kujua matatizo yanayowakabili  wananchi katika jamii.

    Akizungumza baada ya kupokea Mpango kazi wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi kwa Serikali ya Mkoa wa Mjini Maghari katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kikwajuni Mjini Zanzibar, Dk. Shein amesema ni wajibu wa kila kiongozi kutekeleza ilani ya CCM hivyo si vyema kwa baadhi ya mawazi kukwepa kuhudhuria Ziara zinazoendelea jambo linalowakosesha wananchi haki zao za msingi.

    Amesema ziara Zinazoendele katika mkoa huo imekusudia kuangalia miradi mbalimbali ya  maendeleo ambayo inatekelezwa na  serikali kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, ili kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi hiyo katika jamii pamoja na kuimarisha amendeleo katika Nchi.

    Wakati huo huo Dk. Shein amefungua Tawi la CCM Muembe Matarumbeta na kuwataka Viongozi wa tawi hilo kulitumia tawi kwa kukiendeleza chama pamoja na kuwa watekelezaji wa ahadi za wananchi katika kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI