Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na watendaji pamoja na
wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake (hawapo
pichani) katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Prof. James Mdoe.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akielezea mafanikio ya
sekta za nishati na madini nchini katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji na wafanyakazi
kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia
maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Mjiolojia kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Ezekiel Seni akitoa maoni yake katika kikao hicho.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Joseph Mtui akielezea mikakati ya uboreshaji wa chuo hicho katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji Janabi akitoa mchango wake kwenye mkutano huo
Mkurugenzi kutoka Idara ya Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini, Amon MacAchayo akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philip Mathayo akifafanua jambo katika kikao hicho
……………………..
Leo tarehe 21 Agosti 2017 jijini
Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani
amefanya kikao cha kazi na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini
pamoja na Taasisi ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme la Tanzania
(TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya
Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa
Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Chuo cha Madini Dodoma (MRI),
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni
kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara.
No comments:
Post a Comment