• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 24 August 2017

    DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA


     Mkuu wa
    wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
     Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
    viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga
     mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji
     katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi mkoani iringa akiwa sambasamba na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla wakielekea kukagua chanzo kipya cha maji kwa ajili ya wananchi wa mji mdogo wa mafinga
     
    Na Fredy Mgunda,Iringa
     
    Halmashauri ya wilaya ya
    kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji
    mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827
    kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto
    hiyo.
     
    Akizungumza wakati wa ziara
    ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye
    ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa
    wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa
    Ilula.
     
    “Leo nimefika hadi huku
    kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda
    mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani
    ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua
    matatizo ya wananchi”alisema Masenza
     
    Aidha Masenza alisema kuwa
    wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania
    dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi
    wake.
     
    Kwa upande wake mkuu wa
    wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa
    uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka
    kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha
    wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.
     
    Abdallah alisema kuwa
    wananchi wa mji mdogo wa Ilula unamahitaji makubwa ya matumizi ya maji ambapo
    kwa siku wanahitaji maji ya mita za ujazo 2687 kwa siku hivyo hadi sasa
    kunaupungufu wa mita za ujazo 1545 kwa siku.
     
    “Mji huu unakuwa kwa kasi
    kubwa hivyo matumizi ya maji yamekuwa makubwa mno ndio maana tumeanza  kujenga chanzo kingine ambacho kitakuwa na
    suluhisho kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula na kutaua kabisa tatizo la maji”
    alisema Abdallah 
     
    Abdallah aliwataka wananchi
    na viongozi wa ngazi zote kuacha tabia ya kuharibu vyazo vya maji na mazingira
    kwa ujumla hivyo atakaye kamatwa anafanya uhalibifu wowote ule sheria itachukua
    mkondo wake.
     
    “Ni malufuku kwa wakulima
    kulima kwenye vyanzo vya maji,wafugaji kufujia mifugo kwenye vyanzo vya maji
    pamoja na ukaji wa miti hovyo hapo nitakuwa mkali sana kwa watu ambao watakiuka
    haya nayoyasema hii leo kwa kuwa kila kitu kipo kisheria “ alisema Abdallah
     
    Naye meneja wa mamlaka ya
    maji wa mji mdogo wa Ilula Enock Ngoyinde aliiomba serikali ya na kamati ya
    siasa ya mkoa wa iringa kusaidia upatikanaji wa pesa kwa wakati za kumaliza
    mradi huu wa maji ili wananchi waanze kupata huduma bora mapema iwezekanavyo.
     
    Ngoyinde alisema kuwa mradi
    huo ukikamilika utakuwa umeongeza eneo la utoaji wa huduma vya maji kutoka
    wastani wa asilimia 62 hadi asilimia 75 na kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu
    ishirini na tano (25000) ambao watakuwa na mtandao wa bomba za maji

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI