Afisa muandamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah (katikati waliokaa)akifuatilia
kwa karibu wakati wa droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya
Jishindie na DStv ambapo wateja takriban 100 wa DStv walijishindia
zawadi mbalimbali. Kulia ni Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice
Tanzania Hilda Nakajumo, Wengine ni maafisa wa Multichoice Erick Mosha
(aliyesimama) na Leyla Partick.
Afisa muandamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Kushoto akifuatilia kwa karibu
wakati wa droo ya kuchagua washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv
ambapo wateja takriban 100 wa DStv walijishindia zawadi mbalimbali.
Katikati ni Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda
Nakajumo na kulia ni Meneja wa Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Barka
Shelukindo..
……………………………………………………….
Wateja 76 wa DStv wamejinyakulia
zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika promosheni
inayoendelea ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv anapata fursa
ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa mangalau miezi
miwili mfululizo.
Kati ya washindi hao 25
wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora ambavyo ni ving’amuzi
vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi watatu wamejishindia
Kifurushi cha Premium cha Tsh 184,000) cha mwezi mmoja, wengine watatu
Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 122 500), huku washindi 10 wakishinda
kifurushi cha Compact cha Tsh 82,250), 10 kifurushi cha Famili (42,900)
na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,975.
Promosheni hii inaendelea kwa
muda wa miezi miwili itatoa washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo
vifurushi vya muda wa matangazo, ving’amuzi, pamoja na zawadi kubwa
kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar kwa washindi wawili
pamoja na familia zao.
Akizungumza baada ya kuchezeshwa
kwa droo ya kwanza leo hii katika ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja
wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa Zaidi ya wateja elfu
10 wameshiriki kwenye droo hiyo hii ikionyesha muitikio mkubwa wa
wateja.
Pia amebainisha kuwa washindi
waliopatikan katika droo ya kwanza wametoka kila pembe ya nchi ikiwemo
Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mwanza
na Morogoro.
Amewataka wateja wa DStv
kuendelea kulipia ving’amuzi vyao kwani bado droo moja kubwa ya mwisho
ambapo kuna wateja wawili watakaoshinda safari ya kutalii Zanzibar
pamoja na familia zao.
Amesema promosheni hiyo haina
ugumu wa kushiriki kwani anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia kifurushi
chochote kile cha DStv na kisha kuendelea kutumia huduma hiyo na moja
kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo zitakazochezeshwa kila baada ya
wiki mbili. Droo kubwa ya mwisho tarehe 1/9/2017
No comments:
Post a Comment