Leo hii Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshiriki katika uzinduzi wa maonesho ya nanenane yanayofanyika leo kikanda katika Mkoa wa Morogoro viwanja vya Nanenane Mwalimu Julius Nyerere,ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri Maliasili na Utalii Mh.Profesa.Jumanne Maghembe.
Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo ni miongoni mwa Halmashauri mpya iliyofanikiwa
kushiriki maonesho haya licha ya upya wake tayari ina eneo lake kama
Halmashauri katika viwanja hivyo ambapo katika kipindi kifupi tayari
kuna vipando vya aina mbalimbali,bwawa la samaki,mabanda ya kisasa ya
ufugaji wa n'gombe,mbuzi,kuku,bata bila kusahau green house iliyoshamiri
vipando n.k.
Akiongea
katika maonesho hayo mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob amesema
uamuzi wa serikali kuleta maonesho haya umesaidia katika uboreshaji wa
kilimo na inawapa fursa wajasiriamali kujulikana na kujitangaza kisha
kuinua uchumi,pia wananchi kupata elimu ya kilimo kwa ujumla wake.Pia
amewataka wananchi kuendelea kuja kujionea mambo tofauti na mazuri
yaliyofanywa kwa kipindi kifupi katika banda la Ubungo.Amewataka
wananchi wajiyokeze kwa wiki yote hii ya maadhimisho mpaka siku ya
kilele ambayo ni tarehe 8/8/2017.
Nae
Kaimu Mkurugenzi Ally J Ally akizungumza mara baada ya uzinduzi
amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kujionea mambo mazuri yaliyoko
katika banda la Halmashauri ya Manispaa ya ubungo.
Katika
banda hilo la Manispaa wananchi wamepata fursa ya kujionea wataalamu
mbalimbali na kupewa elimu juu ya utengenezaji na usindikaji wa
vyakula,ufugaji kwa ujumla wake,mbinu za kisayansi katika kusafisha maji
yenye tope na kuwa safi na salama kwa kunywa,ufugaji wa samaki wa
kisasa ambapo wamejionea bwawa linalotumika kufugia samaki hao mubashara
likiwa na samaki,pia sehemu za machinjio ya kisasa na kadharika.
Baadhi
ya wananchi waliohojiwa wamesema wanapongeza Halmashauri hii kwa
utendaji uliotukuka kwani mambo wanayoyaona kwenye banda hili hayafanani
na muda mfupi wa Manispaa hii toka ianzishwe,kwani mambo mazuri
yamefanyika katika kipindi kifupi hii inadhihirisha utendaji mzuri wa
kazi chini ya Uongozi wa Mkurugenzi John L.Kayombo.
Maonesho
haya ya Kikanda yameshirikisha mikoa ya Tanga,Dar es
salaam,Morogoro,Pwani.Kauli mbiu ya maonesho haya kwa mwaka huu
ni"
ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ILI
KUFIKIA UCHUMI WA KATI.

HONGERA WAKULIMA
HONGERA MANISPAA YA UBUNGO
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO UMC
No comments:
Post a Comment