• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 31 July 2017

    KENYA;MENEJA WA TUME YA UCHAGUZI AFARIKI


    Meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi Meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha City mjini Nairobi
    Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.
    Mwili wa Christopher Chege Musando, ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi wa masuala ya teknolojia wa IEBC, umepatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti jijini Nairobi
    Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
    Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
    Polisi wanasema kuwa mwili wa afisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo vviungani mwa mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.
    Mkurugenzi mkuu wa IEBC Ezra Chiloba (kushoto) akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City 
    Mkurugenzi mkuu wa IEBC Ezra Chiloba (kushoto) akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City
    Bwana Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vya eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.
    Taarifa zinasema kuwa mwili wa Musando ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Jumamosi asubuhi na watu waliojitambulisha kuwa maafisa wa polisi.
    Tume ya IEBC, ambayo ilitangaza kutoweka kwake Jumapili, haijatoa taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kupatikana kwa mwili wake.
    Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba hata hivyo amefika katika ufuo huo kutoa rambirambi kwa jamaa na marafiki wa marehemu waliofika kuuona mwili huo.
    Mwili wa Bw Musando umesafirishwa hadi chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee Funeral Home.
    Mwili wa Musando ukiwekwa kwenye gari kupelekwa Lee Funeral Home
    Mwili wa Musando ukiwekwa kwenye gari kupelekwa Lee Funeral Home

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI