• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 21 August 2017

    HOSPITAL YA AMANA WAMNASA DAKTARI FEKI

    Aliejifanya dokta feki akamatwa tena Amana akijifanya daktari na wakala wa ajira

    Daktari feki aliyewahi kukamatwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jully 19 mwaka huu amekamatwa tena leo akijifanya daktari katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.



    Akizungumza Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Msimamizi wa huduma kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi Dkt SHANI MWALUKA amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna mtu anajifanya daktari ambaye aliwaahidi wagonjwa kuwa angewapatia huduma na akataka apewe fedha ndipo uongozi wa hospitali hiyo ulipomwekea mtego na kumnasa daktari feki huyo ambaye hakuwa na kielelezo chochote kuwa yeye ni mtumishi wa hospitali ya amana.


    Nao baadhi ya watu ambao wamewahi kutapeliwa na daktari huyo wamesema kuwa amekuwa akijitambulisha kama Dk Abdalah Omary na aliwaahidi kuwasaidia kupata kazi katika mahoteli na makampuni ya ujenzi hiyo na kupewa kiasi cha shilingi laki nane ambazo aliwatapeli na baadaye kuwataka wakutane Amana hospitali Leo  ndipo walipomwekea mtego huo na kufanikiasha kunaswa kwake

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI