Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, akionyesha mfano wa miguu ya bandia leo jijini Dar es salaam. |
Kutokana na sababu za wananchi wengi waishio mkoa wa Dar es salaam kutokua na uwezo wa kumudu gharama za manunuzi ya miguu ya bandia pindi wanapopata ajari na kukatika miguu hali ambayo imempelekea mkuu wa mkoa wa Dar es salaam paul makonda kusaidia nwananchi wake wasio na uwezo wa kumudu gharama za vifaa hivyo, ambapo atawapatia miguu hiyo bure.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amewataka walemavu hao kujitokeza siku ya tarehe 14 na 15 kujiandikisha na kupimwa ili waweze kupatiwa miguu hiyo ya bandia itakayo wasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
"nimefanikiwa, na namshukuru mwenyezimungu nimepata wadau ambao wamenipatia miguu hiyo itakayo wasaidia wananchi wangu mia mbili (200) kwa awamu ya kwanza ambapo watapatiwa miguu hii ya bandia na kuweza kutupa magongo yao na kurejea katika shughuli zao" Alisema Makonda.
Amesema Mguu mmoja unagharama ya hadi Sh. Milioni tatu, ambapo kwa watu mia mbili ni zaidi ya shilingi milioni mia nane.
Aidha amewaomba wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wenye mahitaji na wenye kila sababu ya kuona umuhimu wa fursa hii,kuwa ifikapo siku ya 14 na 15 ya mwezi augost mwaka huu kujitokeza katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ili kupimwa ambapo kutakuwa na wataalamu (Madaktari) watakao chukua vipimo iliwawatengenezee miguu kulingana na mahitaji.
"Hatuwezi kutengeza miguu ili mtu ajaribishie wakati hajapimwa ,nimeona ni vyema wapimwe kwanza ili waweze kupatiwa hiyo miguu na iwasaidie kuweza kutumia katika matumizi yao tunatamani kuona wanarudi tena na siku moja wamshukuru Rais Magufuli kwa kazi kubwa wanao ifanya ya kuwahudumia wananchi wote hasa wanyonge na maskini "Alisema Makonda.
Amesema kwa sasa huduma hiyo itatolewa kwa watu mia mbili tu na baadae itarudiwa tena kwa awamu ya Pili ili kuhakikisha kila mwananchi mnyonge anafikiwa na huduma hii
No comments:
Post a Comment