Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella leo
August 10, 2017 ameamuru makampuni ya Skysraper na Caspian kurudisha
funguo za kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries Limied Mwanza kwa Serikali
na kuwa mali ya Serikali rasmi.
Kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries ni
miongoni mwa viwanda vilivyobinafsishwa wakati wa ubinafsishaji
wawekezaji wake wakiwa Makampuni ya Skyscraper na Caspian lakini sasa
kimefungwa baada ya wawekezaji hao kushindwa kuendeleza uzalishaji kwa
muda mrefu na kuwa eneo la kutunzia vyuma chakavu.
Kwa mujibu wa Bodi ya taifa takwimu mkoa
wa Mwanza unaonesha unaviwanda vipatavyo1,470, huku viwanda vine vikiwa
vimeajiri zaidi ya watu 500, saba vimeajiri watu kati ya 100 - 499, na
viwanda vilivyo ajiri watu kati ya 50-99 vipo 8, viwanda vingine ni vile
vilivyo ajiri kati ya watu 20-49 ambavyo idadi yake ni13, kwaupande wa
viwnda vilivyo ajiri kati ya watu10-19 viwanda 22 na vile vilivyo ajiri
kati watu ya 4-9 vikiwa ni viwanda 279 na mwisho kabisa ni viwanda
vyenye watu kati ya 1-4 hivi jumla yake ni viwanda 1,074.
No comments:
Post a Comment