Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa
10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi
Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya
China.
Hatua hiyo
inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi
la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya
Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini
ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa
Pikipiki hizo.
Makonda
amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la
Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo
hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500 Pikipiki za kawaida 200
Computer 100 Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari
ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.
Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya
Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na
wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi
kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.
Agizo
hilo limekuja baada ya hivi juzi msamariamwema kutoa taarifa za uwepo
wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika kwenye Hotel
wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa akaachiliwa na
kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada
ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabainu Askari hao.
Pamoja
na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake
kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi
cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume
Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo hivyo votendeke kwenye
Mkoa wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki vitendeke.
Makonda
kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa
China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi
wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.
Amesema
hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa
Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi
kushindwa kutoa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment