Katika kile kinachoonekana
kutekeleza dhana ya ‘hapa kazi tu’, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa
Kitila Mkumbo akipanda juu ya tanki kuchungulia maji katika vyanzo vya
maji kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji
Profesa Kitila Mkumbo akiambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt
Angelina M Lutambi(katikati) na Mhandisi wa maji SUWASA Robert Sunday
(kushoto), wakikangua vyanzo vya maji kijiji cha Mwankoko Mnispaa ya
Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa
Kitila Mkumbo (wa pili kulia) akipewa ufafanuzi wa mashine ya kupampu
maji katika chanzo cha maji cha kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida
na Mhandisi wa SUWASA Patrick Nzamba
Katibu Mkuu Wizara ya Maji
Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watumishi watumishi wa Mamlaka ya
SUWASA, bonde la maji la kati na maabara mjini hapa. Wa kwanza kulia ni
Mhandisi SUWASA, Patrick Nzamba.
Mhaidrolojia bonde la maji la kati
Robert Sunday akichangia hoja kwenye mkutano ulioitishwa kwa ajili ya
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuzungumza na watumishi
wa SUWASA, bonde la maji kati na maabara.
……………………………………
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amezihimiza mamlaka za maji
na mabonde ya maji kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia
kujiendesha vyenyewe bila kutegemea serikali kuu.
Profesa
Mkumbo ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya
maji Singida (SUWASA), Bonde la maji kanda ya kati na maabara, mjini
hapa mjini .
Amesema
Serikali haina fedha za kukidhi mahitaji yote ya mamlaka za maji na
mabonde nchini hivyo ni vema vikaweka mikakati ya kujitengemea kimapato.
“Duniani
kote hata Marekani haitoi fedha kwa taasisi kama hizi zenu. Tumieni
kalamu na akili zenu kwa ajili ya kuandika maandiko yatakayowasaidia
kupata fedha za kujiendesha bila kutegemea serikali au wafadhili”,
amesisitiza.
Akisisitiza
zaidi, kwa kusema umefika wakati sasa mamlaka na mabonde ya maji,
zifikirie kuwekeza na kujiwekea mipango thabiti ya kuongeza mapato yao.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo amewataka watumishi wa SUWASA, kutoa huduma bora
itakayovutia wananchi wengi zaidi kupata huduma ya maji katika mamlaka
hiyo.
“Wateja
wa maji ndio wanaowalipa ninyi mishahara na stahiki zingine. SUWASA
ikiwa na wateja wachache kwa vyo vyote uendeshaji wake utakuwa mgumu na
hivyo hivyo upatikanaji wa mishahara yenu nao utakuwa mgumu”, amesema
Profesa Mkumbo.
Ameongeza kuwa SUWASA na mamlaka nyingine za maji nchini ni lazima ziwe na mkakati wa kupanua wigo wa wateja.
“Utamaduni
wa kutoa huduma bora unamfurahisha mteja na atapenda kuendelea kuwa
mteja wa SUWASA wakati wote. Pia itawavutia watu wengi kukimbilia huduma
bora zinazotolewa na SUWASA”,alisema.
Katika
hatua nyingine, Profesa Mkumbo ametumia nafasi hiyo kusisitiza
utaratibu wa kulipia kwanza (pree paid) maji kabla ya kupata huduma ya
maji.
Amesema
utaratibu huo utasaidia kuepukana na wateja wakorofi ambao huzalisha
madeni sugu na kusababisha mamlaka kushindwa kutoa huduma zinazokidhi
mahitaji ya wateja.
“Kupitia
utaratibu huu mteja husika ni lazima ajue matumizi yake ya maji kwa
kipindi cha mwezi. Baada ya hapo analipia kiwango hicho cha maji halafu
ndipo apewe maji ya kiwango alicholipia”, amesema katibu mkuu huyo.
Awali
Afisa Maji bonde la kati Benard Chikarabhani amesema wameanza
utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la Farkwa kwa lengo la kuongeza
usambazaji wa maji katika mji wa Dodoma, Bahi, Chamwino na halmashauri
ya wilaya Chemba.
“Bwawa
hilo linatarajiwa kuwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo 470,000,000
na litachukua eneo la kilometa za mraba 68 pia bwawa litatumika
kuboresha kilimo cha umwangiliaji katika mradi wa umwangilaji Bahi”,
amesema Chikarabhani.
Wakati
huo huo, Chikarabhani amesema bodi ya maji bonde la kati inatarajia
kutumia zaidi ya shilingi bilioni 2.4 kugharamia ujenzi wa ofisi makao
makuu mjini hapa.
“Fedha
hizo zitagharamia pia ukarabati wa ofisi na maabara katika ofisi ndogo
ya bodi zilizopo mkoani Shinyanga. Vile vile ujenzi wa ofisi ya jumuiya
ya watumijai maji ya Mto wa Mbu”, amesema afisa huyo.
No comments:
Post a Comment