• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 10 August 2017



    Na Mary Mafuru TSJ
        Chuo cha uandishi wa habari ( TSJ) kilichopo ilala Sherrif Shamba jijini Dar es Salaam,kinatarajia kuwa na ziara ya kimasomo mwanzoni wa mwezi wa kumi mwaka huu.

      Akizungumza na moja ya  mwandishi  wa blog hii, Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa chuo hicho hapo jana bwana Antony John Mwesongo, amesema kuwa wanatarajia kuwa na ziara hiyo mkoani Tanga ambapo watatembelea sehemu mbalimbali za mkoa huo kwa lengo la kujifunza ikiwemo Mapango ya Amboni na baadhi ya  vyombo vya habari kwani chuo chao kimebeba tasnia ya habari kwa ujumla.

      Lakini pia aliongeza na kusema, bado hawajatoa rasmi taarifa hiyo kwa wanafunzi ambao wapo tayari kwenda kujifunza huko kutokana na kuanza kwa kufanya tafiti kwenye sehemu hizo watakazotembelea na kujua gharama zitakazoweza kutosha kuanzia kwenye malazi,usafiri pamoja na chakula kwenye mkoa huo ukilinganisha na hali ya uchumi ya sasa.

       "Kuna baadhi ya wanafunzi wapo kwenye kujifunza kwa vitendo (Field) ningeomba waweze kuwapa taarifa mapema wazazi wao ili waweze kushiriki kimamilifu ziara hii kwani ni moja ya kujifunza"Alisema Antony John.

      Aidha waziri huyo amesema wazazi wawape fursa watoto wao kwa kushiriki kikamilifu katika ziara hiyo ya kimasomo ili waweze kujifunza kwa vitendo mambo mbalimbali yanayohusu tasnia ya uandishi wa habari kwa ujumla.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI