Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye
tamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kampuni ya mafuta ya
Camel Oil iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha
sekta ya Afya.
Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema
amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya
katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika lengo likiwa ni kuhakikisha
Wananchi wanapata huduma bora za afya.“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ilimradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri. Na siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Magufuli. Sisi tunataka Maendeleo na maendeleo hayana chama,dini wala kabila. Jukumu la kuuendeleza Mji huu wa Dar es salaam ni jukumu letu sote kama wakazi na wananchi wa mkoa huu” Alisema Makonda.
Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kina mama watatu hadi wanne
No comments:
Post a Comment