Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Paul Makonda
ametoa siku tatu kwa mhandisiwa wa umeme wa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha
mchoro wa miundombinu ya umeme ya soko la Bunju B ili Tanesco iweze kuunganisha umeme katika soko
hilo.
Mhe. Makonda
ametoa agizo hilo alipo kuwa akisikiliza kero za wananchi katika viwanja
vya soko hilo baada ya kuelezwa na mhandisi wa Tanesco mkoa wa Tanesco
Kinondoni kuwa manispaa waliagizwa kupeleka mchoro tangu mwezi April mwaka huu lakini
hadi leo hawajafanya hivyo, jambo ambalo limesababisha usumbufu mkubwa kwa
wafanya biashara wanaofanya biashara sokoni hapo.
Pamoja na hayo Rc Makonda amewataka watumishi na
watendaji serikali mkoani humo kufanya kazi kwa bidii na kushughulikia kero na
changamoto za wananchi ilikuweza kuleta maendeleo na kutekeleza ilani ya CCM.
“watendaji tuna mchosha Rais kwa mambo madogomadogo ambayo tungeweza
kuyamaliza sisi huku chini yeye tuka mwacha akashughulikia mabo makubwa ,huyo
huyo ashughulikie makinika , Mafisadi , Bomba la Mafuta halafu sisi tuwe
tumekaatu haiwezekani lazima tuwajibike “alisema Makonda
Kwa upande wao wanachi hao wakizungumza ma mhe. Makonda
katika mkutano wa hadhara wamesema kuwa tatizo kubwa linalo kabili sokohilo ni
ukosefu wa umeme,Maji ya kutosha, uchache wa matundu ya choo na kero ya baadhi ya wafanya biashara
kukimbilia kwenda kufanya kazi barabarani.
Wanachi hao wameomba soko hilo kufanywa sehemu
muhimu ya ya kuuza mazao na bidha kwa jumla ili kupunguza msongamano katika
masoko mengine,na kulifanya soko hilo kuwa enemuhimu la kibiashara pia
itasaidia kuwatoa wote wanaofanya biashara katika maeneo ya pembezoni mwa barabara.
Aidha wananchi hao wameeleza kero ya kupasuka kwa
mabomba ya maji (DAWASCO) ambapo Mhandisi wa Dawasco Bw. Aron Joseph ambapo
amesema kuwa hali hiyo ya kupasuka ni inatokana na masuala ya kiufundi ambapo
kumekuwa na presha (Msukumo) kubwa wa maji kutokana na ukosefu wa matanki ya
kutosha.
Hata hivyo Mhandisi Aron ametoa siku mbili kwa
Meneja Mkoa bagamoyo Meneja wa DAWASCO kanda ya Tegeta na Bagamoyo Edga Zawa
pamoja na Meneja Mkoa Tegeta Ambokile kuhakikisha mabomba yote yanayomwaga maji
yanazibwa haraka ili kuondoa keo kwa wananchi hao.


No comments:
Post a Comment