• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 22 August 2017

    WADAU WA KILIMO CHA PAMBA WAKUTANA NA KUJADILI MBINU ZA KUBORESHA ZAO HILO MKOANI GEITA


    Wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoani Geita pamoja na wabunge na wadau wa Kilimo cha Pamba wakifuatilia kwa makini Mkutano  huo.

    Mkurugenzi
    Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ,Dionis Myinga akijitambulisha mbele ya wadau wa sekta ya kilimo cha pamba.

    Wada wa Kilimo cha Pamba wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano ya kuboresha kilimo hicho.

    Mkuu
    wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza
    kwenye mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba

    Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita ambaye pia anahusika na maswala ya Kilimo,Emmly Kasagara akitoa taarifa ya Kilimo cha pamba Mkoani humo.















         
     ………………………………………………………….
    Zao la biashara la pamba ni moja kati ya muhimili mkubwa wa uchumi nchini na katika
    Mkoa wa Geita lakini kwa miaka ya hivi karibuni limeendelea kupoteza umaarufu kutokana
    na mbegu kutokuwa na ubora pamoja na viuatilifu na bei kutokuwa na mpangilio.
    Hali hii ndio inayosababisha wadau wa pamba wakiwemo Viongozi wa Wilaya,Wabunge ,maafisa
    Kilimo,washauri na wakulima kukutana kwenye ukumbi wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa
    Geita kujadili namna wanavyoweza kuendelea kuinua kilimo cha pamba ili kuwa na
    faida kwa mkulima na mnunuzi.
    Katika Mkutano huo Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu
    Ezekiel Kyunga amesisitiza kwa wadau wa kilimo cha pamba kuwa kila mmoja
    anawajibu wa kuhakikisha kuwa kilimo hicho kinarudi na kinafufuliwa katika
    ubora wake uliokuwepo miaka ya nyuma.
    “Tunawajibu wa kuhakikisha kwamba kilimo hiki kinarudi kwenye ubora wake na hakuna
    kinachoshindikana ni sisi kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kurejea historia
    kwani itatusaidia”Alisema Kyunga.
    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe,Safari Nicas Mayala,ameelezea sababu za zao
    la pamba kuanguka ni kukosa mtu anayeweza kuhudumia na kwamba zamani vyama vya
    ushirika vilikuwa makini katika usambazaji wa mbegu zenye uhakika.
    “Pamba imeanguka baada ya kukosa mtu wa kuihudumia, mtu wa kuhihudumia alikuwa ni
    ushirika vyama vya ushirika hadi miaka ya 1990, sasa hivi wangekuwa wamesambaza
    mbegu ya pamba na dawa na Siyodani na ndio maana hapa mkulima amesema kwamba
    turudishie Siyodani namba 25 ilikuwa inafanya kazi vizuri licha ya kupingwa
    marufuku kutokana na uharibifu wa mazingira”Alisisitiza Mayala.
    Akifunga Mkutano huo Mkuu wa Mkoa Ezekiel Kyunga,amesisitiza kuwa suala la umoja wa wanunuzi
    wa zao la Pamba, UMWAPA halipo kwani walipatiwa ridhaa ya mwaka mmoja kama
    majaribio na Waziri ambaye alikuwa madarakani kwa miaka hiyo na kwamba
    walipatiwa wafanye kazi kwa majaribio kwa mwaka mmoja  na wameshapatiwa maelekezo ya kutowakandamiza
    wakulima kupitia UMWAPA.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI