katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu leo.
Naibu Waziri Mpina
akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya kuongea na baadhi
ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu jimboni kisesa leo.
Baadhi ya wakulima wa Pamba
wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
(hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika kijiji cha Mwabusalu
mapema leo.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa
Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba kijijini Mwabusalu, Meatu
Mkoani Simiyu leo.
………………………….
NA EVELYN MKOKOI – MWABUSALU MEATU
Hatua kali zitachuliwa kwa
wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu wa zao la Pamba
nchini, Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
alipokuwa akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata
ya Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake jimboni
Kisesa.
Mpina
alisema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la
Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi
kabisa katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo na kuwataka
watu hao kuwaletea wakulima dawa bora kabisa na kinyume na hapo wizara
husika itachukua hatua dhidi yao.
Aidha amewataka wakulima wa kijiji
hicho kinacholima zao hilo la mfano nakutoa mbegu Bora Pekee ya pamba
nchini kuacha kilimo cha mazoea na kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza
maeneo wanayoishi kutokana na faida itokanayo na biashara ya zao la
pamba kuninunulia chakula cha kutosha na kutoka kwenye nyumba za tembe
na kujenga nyumba za kisasa.
Sambamba na hilo Mpina
amewataka wakulima hao kuzingatia sauala la utunzaji wa mazingira kwa
kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia changamoto ya
mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.
Awali, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Pamba cha Geki Investiment limited
na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema mwakani
ili wakulima wa kata ya Mwabusalu waweze kunufaika kutokanana mauzo ya
pamba yao karibu. “Serikali hii inalenga katika kuinua na kuimarisha
uchumi wa viwanda hivyo kiwanda hiki sasa wakati umefika wakuanza
uzalishaji kisikae hapa na kutumika kama ghala kianze kazi mara moja,
vinginevyo hatuta mvumilia muwekezaji huyu kama atashindwa Wizara husika
itafanya kazi yake”. Alisisitiza Mpina.
Serikai ya awamu ya tano toka
iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba kutoka bei ya awali ya
shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200 imeelezwa kuwa kata ya
Mwabusalu, ni kata ambayo imepata upendeleo kwa wakulima kuuza Pamba
hiyo kwa kiasi cha shilingi 1,320 kwa kilo.
Tafiti zinaonyesha kuwa kata ya
Mwabusalu inalima Pamba ambayo pamoja namatumizi mengine inatoa Mbegu
ambayo inapatika pia katika maeneo mawili tuu nchini yanii mwabusalu na
Ingunga Mkoani Tabora
No comments:
Post a Comment