Mmoja wa wananchi wa Lindi akipata maelekezo toka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA, Bi. Rose Mdami.
Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika viwanja ya Ngongo, karibu kabisa na Jukwaa Kuu la Maonyesho.
Baadhi ya Wananchi waliotembelea
Banda la NIDA wakifuatilia maelelezo ya namna ya kujisajili toka kwa
Afisa Usajili mkoa wa Lindi Ndugu Oliver Walles Mahinya.
Kikundi cha jadi kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Nanenane Viwanja vya Ngongo Lindi.
Wananchi wa Mkoa wa Lindi
waliojitokeza kushuhudia uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Kitaifa ya
Nananenane yanayofanyika mkoani humo kwenye viwanja vya Ngongo.
Maonyesho ya Nanenane yaliasisiwa mwaka 1990 mkoani Mbeya na yameendelea
kwa mzunguko kwa kila mkoa kupata fursa ya kuandaa na kushiriki.
……………………..
- WANANCHI KUPATA VITAMBULISHO VYAO NDANI YA MUDA MFUPI
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA)ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zinazoshiriki maonyesho ya
Kitaifa ya Nanenane, yanayofanyika katika Mkoa wa Lindi katika viwanja
vya Ngongo.
Maonyesho hayo ambayo
yamezinduliwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George
Simbachawene; ambaye amewaasili na kukagua baadhi ya mabanda kabla
kuwahutubia wananchi wa Lindi waliokusanyika kwa wingi kushuhudia tukio
hilo.
NIDA inashiriki kwenye maonyesho
hayo kwa kutoa huduma ya Usajili kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi ambapo
kwa wale watakaokamilisha taratibu zote za Usajili watapatiwa
Vitambulisho vyao ndani ya mwezi mmoja. Huduma nyingine zinazotolewa ni
pamoja na Ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ambao
walisajiliwa kwenye maonyesho hayo mwaka Jana, wananchi kupata taarifa
za vitambulisho vyao kwa wale ambao wamekamilisha taratibu za Usajili,
elimu kuhusu matumizi, faida na umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa pamoja
na kusoma taarifa za mwananchi kwenye Kitambulisho chake kutumia Tovuti
Salama iliyoundwa kurahisisha matumizi ya vitambulisho vya Taifa.
Kauli Mbiu ya maonyesho hayo kwa
mwaka huu “Zalisha kwa Tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi
ili kufikia uchumi wa kati”. Ili kufikia malengo haya; kupitia mfumo wa
Taifa wa Usajili na Utambuzi wa Watu kuwatambua Wakulima na Wafugaji,
uzalishaji wenye tija na ufugaji wa kisasa unawezekana. Hivyo wananchi
wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa
mapana ya mfumo huu katika kuinua uchumi na maendeleo ya Taifa.
Maonyesho ya Nanenane Kitaifa
yanafanyika kwa awamu ya Nne mkoani Lindi ili kutoa fursa pana kwa
wakulima na wafugaji kunufaika na elimu pana inayotolewa na Taasisi na
Mashirika mbalimbali kwa lengo la kufanikisha ndoto kubwa ya Taifa la
Uchumi wa Kati
No comments:
Post a Comment