Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar (ZURA) Haji Kali Haji
akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na hali ya upatikanaji wa
mafuta Zanzibar huko Ofisini kwake Maisara Zanzibar
Picha na Kijakazi Abdalla –Maelezo
……………………
Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar
MKURUGENZI Mkuu Mamlaka Ya
Udhibiti Wa Huduma Za Nishati Na Maji Zanzibar(ZURA) Haji Kali Haji
aliwataka wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu tatizo la upungufu wa mafuta
nchini kuwa yapo ya kutosha.
Alisema mafuta yapo ya kutosha
ingawa kwa siku mbili kulijitokeza upungufu wa mafuta aina ya dizeli na
hii ni kutokana na kazi ya usambazaji katika wa mafuta hayo katika
vituo.
Akizungumza na waandishi wa habari
hizi huko ofisini kwake Maisara amesema wananchi hawatokuwa na tatizo
hilo kwa upande wa dizeli na kuahidi baada ya siku mbili tatizo hili
litaondoka kabisa.
“ Hali ya sasa ya mafuta hapa
Zanzibar itaendelea kuweko na hawategemei kuadimika badala ya kuwepo
mafuta ya kutosha na kuweza wananchi kujipatia huduma hii bila
usumbufu”Alieleza mkurugenzi huyo.
Aidha alisema kwa upande wa
Kampuni ya GAPCO mafuta aina ya dizeli yapo lita 39,112 na vile vile
watapokea mafuta mengine yaliyokuwa ya kampuni Zanzibar Petrolium (ZP)
LITA 168,000 za dizeli.
Pia amesema kwa upande wa Petrol
kampuni hiyo ya Gapco ina lita 405,000, na kwa upande wa Kampuni United
Group kwa mwezi huu wa Septemba ina lita 2,267,000 za Petrol na lita
1,91,424 za mafuta aina yaq dizeli na mafuta ya taa lita 629,000.
Kwa upande wa kampuni ya Zanzibar
Petrolium (ZP) Mkurugenzi amesema lita 7,000,00 za Petrol wakati Dizeli
kampuni hiyo ina lita 800,000 na kwa upande wa mafuta ya taa wana lita
250,000.
Akiendelea kwa kusema katika mwezi
wa Oktoba Kampuni ya ZP watakuwa na lita 1,200,000 za Petrol wakati
mafuta ya dizeli watakuwa na lita 800,000 na mafuta ya taa lita 250,
000.
Amesema kwa kipindi hiki cha miezi
miwili Kampuni ya AUGUSTA ENERGY kutoka Switzerland iliyoshinda zabuni
ya uletaji mafuta Zanzibar itaingiza mafuta jumla ya lita 9,57,116 za
Petrol na lita 7,867.538 za mafuta aina ya dizeli.
Na kwa upande wa Pemba , MT Ukombozi ilishusha mafuta lita 360,000 za dizeli na lita 400,000za mafuta ya Petrol.
Mkurugenzi huyo amesema kwa upande wa mafuta ya ndege Kampuni ya PUMA imeingiza jumla ya lita 2,300,000 kwa mwezi huu .
Pia amewahakikishia wananchi kuwa
hawatopata usumbufu tena tayari Kampuni ya AUGUSTA ENERGY imeleta mafuta
ya ziada tani 200 za Petrol na tani 150 za Dizeli mafuta ambayo kwa
sasa yamo katika meli hiyo ikiwa ni ziada ya yale wanayotakiwa kuleta
Zanzibar.
HABARI HII IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment