Na Ahmed Kombo
Watetezi wa haki za binadamu kwa umoja wao wametaka watu
wasiojulikana waweze kuchukuliwa hatua za kiusalama mara moja
ili kubaini wahalifu hao wanajihusisha na vitendo vya
kikatili dhidi
ya watu mbalimbali na kuzuia hali hiyo isiendelee
kutokea tena.
Akisoma tamko hilo leo kwa niaba ya wadau wengine
jijini Dar es Salaam mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za
binadamu DAKTA HELEN KIJO-BISIMBA amesema katika
kipindi kifupi kumekuwa na matukio
kadhaa ya ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu yakiambatana na vitendo vya
mauaji,utekwaji na manyanyaso kwa watetezi wa haki za binadamu,viongozi wa
kisiasa,maafisa wa polisi na wananchi matukio ambayo yameendelea kuleta hofu
baina ya wananchi kuhusu hali ya usalama nchini.
Dakta KIJO-BISIMBA
amesema wadau pamoja na jumuiya ya watetezi wa haki za binadamu
wanasikitishwa na vitendo hivyo huku wakiwaomba viongozi wa dini wachukue hatua
madhubuti kukemea matukio kama hayo kwa nguvu kwani mwisho wa matukio kama haya
ni kuvunjika kwa amani nchini.
Katika hatua Lhrc
kimefurahishwa na kauli ya Rais Dakta
MAGUFULI ya kuonyesha
kutofurahia adhabu ya kifo,kauli ambayo inalandana na juhudi za haki za
binadamu za kupinga adhabu ya kifo kwa vile inadhihirisha kuwa adhabu hiyo
haina faida na haitekelezeki nchini.
Kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu Tanzania
2016, mpaka kufikia mwaka 2015 jumla ya watu 472 wamehukumiwa kunyongwa wakati
mara ya mwisho kutekelezwa kwa adhabu hiyo ilikuwa mwaka 1994.

No comments:
Post a Comment