Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe Paul Makonda ,meitupia lawama Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Ilala kwa tabia ya kuwavizia wafanyabiashara wakati wa ukusanyaji mizigo, na baadhi yao hudai pesa kinyume cha sheria (rushwa) ili kusamehewa faini wanayotozwa na Mamlaka hiyo.
Hayo
yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika
mkutano wake na Wafanyabiashara wa Dar es aliouitisha kuzungumza nao
ili kutatua kero zao.
"Ninaushahidi
wa clip hapa m fanya kazi wa TRA akiomba milioni 100 katika duka la
mfanyabishara biashara, na ninyi wafanyabiashara Nawaomba mfunge camera
katika maduka yenu ili tuwabaini hao wanao ombarushwa". Amesema
Makonda.
Katika
hatua nyingine Makonda amewaomba wafanyabiashara kuchangia kampeni
yake ya ujenzi wa vyoo vya shule na Ofisi za walimu katika mkoa wa Dar
es Salaam, ambapo pia aliwataka na kuunda Kamati kwaajili ya kujadili
maendeleo yao kibiashara na changamoto za kazi yao.
Mkuu
wa kodi mkoa wa kodi Ilala Abdull Mapembe, amesema Kuna baadhi ya
wafanyabiashara wa sio waaminifu huzunguka na lisiti moja, pia huandika
bei tofauti na thamani hali si ya bidhaa katika risiti ya kielektroniki.
"Ikiwa
Mfanyabiashara atabainika kuwepo kulipa kodi au kuandika lisiti kwa
kuficha gharama hali si ya mazoez ya bidhaa atachukuliwa hatua za
kisheria." Amesema Afisa huyo.
Katika
upande mwinginw kumezuka lawama kwa wafanyabiashara wa vifaa na spea za
magari kwa kusema jeshi la polisi limekuwa likichukua spea hizo kwa
kusema miongoni mwa vifaa hivyo ni vya wizi hali ambayo wafanya biashara
hao wamesema hakuna ukweli wowote ambapo wamemwomba mhe. Makonda kutoa
utaratibu kwa Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam
ilikurudisha vifaa hivyo vya magari ambavyo havijachukuliwa na wananchi ,
nakusema kuwa hii inaonyesha kuwa havikuwa vya wizi hivyo ni haki
kurudishiwa wenyewe.

No comments:
Post a Comment