Na Masanja Mabula -Pemba ..
MAHAKAMA
kuu kanda ya Pemba, chini ya Jaji Mkusa Isac Sepetu, hatimae imempa
dhamana mwanamke mwenye mtoto wa siku 21, anaetuhumiwa kukutwa na kete
3,621 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya.
Jaji
Mkusa, alilazimika kuitisha jalada la kesi hiyo ghafla kwenye kizimba
cha mahakama kuu, baada ya Mahakama ya Mkoa Chakechake, chini ya hakim
Hussein Makame Hussein, kuwanyima dhamana watuhumiwa hao.
Mama
huyo Zuhura Ahmed Ali (29) mkaazi wa Jadida na mwenzake Seif Ali Seif
(30) mkaazi wa Mtemani wote wilaya ya Wete, walipandishwa mahakamani
mbele ya hakimu Hussein na kuwakosesha dhamana.
Licha
ya wathumumiwa hao akiwemo mwanamke huyo, kuangua kilio cha taratibu na
kuiomba mahakama dhamana huku akigonga meza na kushindwa kuitoa,
hatimae Jaji Mkusa baada ya kuitisha jalada la watuhumiwa, hao alimpa
dhamana mwanamke huyo, kwa sababu ya kuwa na kichanga.
Jaji
Mkusa Isac, alilazimika kumpa masharti ya dhamana mtuhumiwa mmoja
pekee, kwa kuandikisha shilingi milioni 5, na wadhamini wawili, wenye
kima kama hicho, masharti ambayo aliyatimiza.
“Zuhuru
tunakupa dhamana ya shilingi milioni tano, na wadhamini wenye kima kama
hicho kila mmoja, lakini mwenzako ataenda rumande hadi tarehe
iliopangwa 20 mwezi huu”,alisema.
Mara
baada ya watuhumiwa hao kupanda juu ya kizimba cha mahakama, Mwendesha
Mashitaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa mashitaka Ramadhan Suleiman
Ramadhan, alidai kuwa wote kwa pamoja, Septemba 9, mwaka huu
walipatikana na dawa hizo za kulevya.
Alidai
kuwa, walipatikana na kete hizo 3,621 kituo cha Polisi Mkoani Pemba,
majira ya saa 6: 45 mchana, mara baada ya kupekuwaliwa, wakijua kuwa
hilo ni kosa.
Mwendesha
mashitaka huyo, aliiambia mahakama hiyo kuwa, kufanya hivyo ni kosa,
kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) sheria no 9 ya mwaka 2009, kama
ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 11 (a) cha sheria no 12 ya
mwaka 2011 sheria ya Zanzibar.
Mara
baada ya kusomewa mashitaka yao, watuhumiwa hao kwa pamoja, walikana
kuhusika na kosa hilo na kuiomba mahakama hiyo, iwapatie dhamana ombi
ambalo kwa mtuhumiwa Seif, lilipingwa na mtuhumiwa Zuhura kukubalika.
Mtuhumiwa
Zuhura Ahemed Ali, aliiomba mahakama hiyo kumpa dhamana, kutokana na
kuwa ananyonyesha mtoto aliejifungua siku 21 zilizopita na kuyatimiza
masharti ya dhamana.
“Muheshimiwa
jaji, naomba unipe dhamana, maana mimi kwanza hali yangu sio nzuri,
lakini kisha nna mtoto mchanga nanyonyesha na tokea juzi ninae Polisi,
na kuna mbu”,aliomba mtuhumiwa huyo.
Kwa
upande wake mtuhumiwa Seif Ali Seif, aliomba dhamana hasa kutokana na
kwamba, yeye hahusiki na tukio hilo, na siku tatu kamili, alikuwa kituo
cha Polisi na hajapata mlo.
“Muheshimwa,
kwa vile mimi sihusiki na tukio hili, naomba dhamana, maana kwanza nna
njaa na hali yangu sio mzuri”,aliomba dhamana hiyo, maombi ambayo
yamekataliwa mahakamani.
Baada
ya maombi hayo ya dhamana Jaji Mkusa wa mahakama kuu, ndipo
alipomuamuru mtuhumiwa Seif, kwenda rumande hadi Septemba 20 mwaka huu.
Aidha
Jaji huyo, alisema kwa vile tayari upelelezi umeshakamilika, siku hiyo
mashahidi wote waitwe na barua za wito zitolewe kwao
No comments:
Post a Comment