• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 26 September 2017

    Mwanasiasa mkubwa aonekana Nchini Kenya


    Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad leo Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.
    Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu. 
    "Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo) ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi" alisema Julius Mtatiro 
    Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI