• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 20 September 2017

    Rais wa Uganda atoa neno vifo vya Watanzania 13 nchini kwake

    Rais wa Uganda  Yoweri Kaguta Museveni amesema upelelezi wa kubaini chanzo cha ajali iliyosababisha vifo vya Watanzania 13 waliokuwa wakitoka harusini nchini humo kuelekea Tanzania bado unaendelea na ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.
    Waziri maalumu wa Jiji la Kampala, Betty Kamya wakati akisoma salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Museveni amesema pamoja na kutoa pole kwa familia, kiongozi huyo ameagiza uchunguzi wa chanzo cha ajali ufanyike.
    Waziri Kamya amewasilisha Salamu hizo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki pamoja na kutoa hati za vifo ambapo amesema “Rais Museven anawashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu cha kupoteza wapendwa wao. Nakabidhi vyeti hivi vya vifo vya ndugu zetu 13 nawapa pole sana,”.
    Aidha Bi Kamya amesema Rais Museveni amewapongeza maharusi, Dk Aneth na Dk Trease Ibingira na amewatakiwa maisha mema ya ndoa, ikiwa ni pamoja na kuwaombea ili waweze kukabiliana na kipindi kigumu walichonacho.
    Kwa upande wa Waziri Kairuki ambaye amepokea miili hiyo kwa niaba ya Rais, amesema Rais Magufuli amepokea taarifa ya vifo hivyo kwa mshtuko na alitoa maelekezo ya kupokewa kwa miili hiyo na kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi Lugalo ili iweze kuagiwa hapo na kusafirishwa kwa maziko.
    Mh. Kairuki amesema kwamba maagizo hayo ya Rais wanaendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa magari kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo.
    Waziri Kairuki amesema kwa namna isiyo katika wakati wa kawaida, anawapongeza maharusi na kuwatakia maisha mema.
    “Haya ni mapenzi ya Mungu, hili lisiwanyong’onyeshe maharusi. Katika wakati usiokuwa wa kawaida nawapongeza maharusi na kuwatakia maisha mema” amesema Kairuki.
    Mbali na hayo Mh. Kairuki ameishukuru Serikali ya Uganda kwa kukodi ndege na  kuirudisha nyumbani miili hiyo ya Watanzania 13 waliofariki kwa ajali nchini Uganda

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI