Serikali ya Uingereza yasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar
Serikali ya Uingereza imefahamisha kusimamisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.
Serikali ya Uingereza ilikuwa ilikuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshş la Myanmar.
Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May ametangaza kuwa serikali yake inasitisha ushirikiano huo wa kijeshi na Myanmar.
Hayo waziri mkuu wa Uingereza aliyafahamisha katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
Theresa May amesema kuwa Uingereza inasikitishwa na vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Myanmar ammapo waislamu wa jamii ya Rohingya ni waathirika.
Aliendelea kusema kuwa Bi Aung San Suu Kyi anatakiwa kutamka wazi kuwa operesheni zinazoendeshwa zisitishwe haraka iwezekanavyo.
Zaidi ya waislamu 421 000 kutoka jamii ya Rohingya wamekimbilia nchini Bangladesh tangu kuzuka kwa mauaji Agosti 25

No comments:
Post a Comment