Pichani ni CEO wa Uhai Production
Ndg. Tido Mhando akimkabidhi mkataba walioingia leo ndg. Festo sanga
Mkurugenzi wa Singida United Football Club.
……………………………………………………….
Ni siku nyingine ya mafanikio
mengine kwa klabu ya Singida United kutokana na kuingia mkataba mnono wa
miaka miatatu (3) wa kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV kupitia Azam Tv.
Akizungumza kwa furaha, Mkurugenzi wa Singida United Football Club Ndg. Festo Sanga amesema “Tunawashukuru Uhai production wanaoendesha Azam Tv kwa kukubali kuanzishwa kwa kipindi cha Singida United Tv kitakachokuwa kinarushwa kupitia Azam Tv.

Ni mafanikio ya kujivunia kuona
kila mkakati tunaoupanga unafikia malengo, tunaendelea kuwaomba
watanzania na wadau wa mpira kuwa tuungane kuleta mabadiliko ya
uendeshaji wa vilabu vyetu na zaidi soka kwa ujumla. “Pia kuanzishwa kwa
SINGIDA UNITED TV ni moja ya njia ya kuwatangaza wadhamini wetu ambao
wamewekeza kwenye club yetu.
No comments:
Post a Comment