• Breaking News

    ..

    ..

    Friday 29 September 2017

    Wakazi wa Monduli wanakunywa maji tangu 1961


    Ikiwa tunaelekea miaka 57 Tangu Tanzania ipate uhuru, wananchi wa kata ya Miserani Wilayani Monduli ambako ndiyo chimbuko la madini Tanzania, bado wanatumia maji machafu kwa matumizi ya kila siku kwenye maisha yao.

    Taarifa hiyo imetolewa na wakazi wa kata hiyo walipokuwa wakizungumza mbele ya timu ya serikali, wakiwaomba kuwasidia upatikanaji wa maji safi na salama karibu, ili kuwapunguzia muda wa kutafuta maji katika mabwawa ambayo sio salama, lakini wanalazimika kuyatumia kwa kunywa na kupikia kwasababu hakuna mengine.

    Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Issack Joseph alipokuwa akiilezea timu ya serikali inayopitia kuandaa mapendekezo ya Muundo wa Kipindi cha pili wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini TASAF waliotembelea wilayani hapo, amesema Halmashauri inafanya juhudi kuondoa changamoto hiyo, lakini kutokana

    na ufinyu wa bajeti wanatekeleza kwa awamu ambayo hata hivyo haitoshelezi mahitaji.
    Timu ya TASAF imepita kwenye kaya hiyo leo kuona na kutathimini ili kuandaa mapendekezo ya kunusuru kaya maskini, walipotembelea mabwawa na kaya zilizoko kwenye mpango huo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI