Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa
Ofisi za Walimu Kanali Charles Mbuge akizungumza katika uzinduzi wa
ufyatuaji tofali za ujenzi wa ofisi za shule katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda akishiriki wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi wa
ofisi za kisasa 402 leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii.
…………………………….
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda leo amezindua rasmi wa Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya ujenzi
wa ofisi za kisasa 402 za Walimu ambapo amewasihi Wadau na Wananchi
kuunga Mkono jitiada hizo.
Katika uzinduzi huo RC Makonda ameshiriki zoezi la Ufyatuaji wa Matofali kwaajili ya Ujenzi huo.
Makonda amesema lengo la Ujenzi wa
Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze
kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.
Amesema wapo wengi waliopanga
kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki
kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati
aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.
RC Makonda ametoa wito kwa
Wananchi na Wadau kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au
Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.
Amesema ataki kuona kwenye Mkoa
wake Walimu wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea
kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.
Aidha amesema hadi sasa
amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji Mashine za
kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga
hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.
Amewaomba Wananchi kuwa na
uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi
vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.
Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa
Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel
Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa
kusaidia katika zoezi hilo.
Katika hatua nyingine RC Makonda
amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili
wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais Dk. John Pombe Magufuli
ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi
sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo
watahakikisha ujenzi huo unakamilika
No comments:
Post a Comment