Mkuu wa Wilaya ya Arusha
Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini
Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo
linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha
Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha
Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa
wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia vitambulisho hivyo
vitawawezesha watanzania kutambulika kila mahala, pamoja na raia wa
kigeni kufanya shughuli zao bila usumbufu ikiwa ni pamoja serikali kuwa
na taarifa sahihi za wananchi.
Aidha amesema kuwa wananchi
wasisubiri mpaka zoezi hilo kufikia tamati ndio kujitokeza Kwa wingi
kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano na usumbufu mkubwa
kwa wananchi.
“Naomba niwafahamishe na kutoa
rai kwa wananchi wangu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili na
wasisibirie siku kubaki chache ndio wajitokeze kwa kuwa kunapelekea
usumbufu mkubwa sana hivyo,zoezi hili pia litakuwa na manufaa makubwa
kwa wananchi”alisema fabian
Pia ametaka kila mwananchi
kushiriki zoezi hilo na kutolihusisha na masuala ya kisiasa kutokana na
umuhimu wake,kwa kuwa lengo ni kutambua na kusajili na kutoa
vitambulisho vya taifa.

Afisa kutoka mamlaka hiyo wilaya
ya Arusha Mjini Juliette Raymond Amesema lengo la zoezi hilo ni
kuwezesha serikali kutambua wananchi wake wapo wapi na wanafanya nini
ilimradi anaishi ndani ya mipaka ya Tanzania ,hivyo zoezi hilo ni
lazima kwa kila mtu kwa Mujibu wa sheria.

Kwa wilaya ya Arusha Mjini zoezi
hilo linaendelea katika kata ya Sombetini,Sekei na Themi ambapo zoezi
hilo linafnyika katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kata ya
Sekei,Themi katika viwanja vya nane nane na Sombetini Ofisi za Mtendaji
kata eneo la Mbauda Sokoni.


No comments:
Post a Comment