Akizungumza hayo wakati wa
uzinduzi wa mradi wa Ukunga salama (More and Better Midwives)
uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bukumbi kilichopo
Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
“Sisi sote tunafahamu umuhimu wa
wauguzi na wakunga katika kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo
Serikali ya awamu ya tano tumejipanga kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa
kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa
Serikali inafahamu kuna changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada
mbalimbali za afya pamoja na nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi
ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile
amewaonya wakunga na wauguzi wenye tabia ya kutumia lugha chafu kwa
wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo
inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya
Misungwi Bw. Juma Sweda amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa
wawe mstari wa mbele katika kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa
gharama nyingi pindi wanapopata maradhi na mpaka hivi sasa wananchi
wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga
Salama nchini Dkt. Julius Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili
wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya
Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa kuwalipia ada pamoja na mahitaji
mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa
Uuguzi na Ukunga katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa na mradi
huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye
masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika
kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa
Ukunga salama unaojulikana kama “More and Better Midwives” ambao
umeshirikisha taasisi isiyo ya Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka
Chama cha wakungwa Canada(CMA) na Chama cha wakungwa Tanzania TAMA pia
alitembelea Zahanati ya Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya
upatikanaji wa dawa .
No comments:
Post a Comment