Kufuatia sintofahamu iliyokuwa inaendelea maeneo ya Mombasa Gongo la Mboto kati ya wananchi na jeshi la polisi na kupelekea baadhi ya raia kujeruhiwa na polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa polisi walikuwa wanalipiza kisasi kufuatia kuuawa kwa askari mmoja wa kikosi cha 'Field Force Unit' (FFU)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ametembelea eneo hilo na kusikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi kuchukua sheria mkononi na kujeruhi watu ambapo ameagiza wote waliohusika kufanya matukio hayo kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Nimeambatana na RPC Salum Hamduni hivyo kwa wale walihusika hatua zitachukuliwa, na wale waliojeruhiwa watatibiwa, pia tumewachukua baadhi ya wananchi ambao wamehaidi kutoa ushirikiano hivyo tutalifanyia uchunguzi na kutenda haki" Alisema DC Mjema.
DC Mjema amewataka wananchi wote walioharibiwa mali zao wajiorodheshe na serikali ya wilaya italifanyia kazi, huku akisisitiza hakukuwa na sababu ya kuchukua sheria mkononi wakati kulikuwa na mbadala wa kulichunguza suala hilo na kulipatia utatuzi.
DC Mjema amewaomba wananchi watulie na waendelee na shughuli zao kwani hilo siyo jambo kubwa la kupelekea watu wauane na wavuruge amani ya nchi.

amesema majira ya saa 12 asubuhi Ukonga jijini Dar es salaam askari wa jeshi hilo wakiwa kazini waliukuta mwili wa askari huyo ukiwa pembeni mwa uzio wa kambi ya Ukonga akiwa ameanguka chini huku pikipiki yake aliyokuwa akiendesha ikiwasha taa za tahadhari na mwili huo ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye paji la uso na sikio moja likiwa limekatwa kabisa.
Amesema polisi kupitia kikosi kazi chake kinaendelea na msako mkali wa ufuatiliaji wa tukio hili la kinyama ili kuwabaini watuhumiwa waliohusika kutekeleza mauaji hayo na kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili. Katika hatua nyingine jeshi hilo limekiri kupokea malalamiko ya watu kupigwa na askari huku akidai vitendo hivyo haviendani na maadili ya jeshi la polisi.
“Jeshi la polisi, limepokea malalamiko ya watu wanaosemekana ni askari kufanya msako na kuwapiga wananchi wanaoishi maeneo ya jirani na kambi ya Polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ambao hawana hatia yeyote. Jeshi la Polisi linalaani vikali vitendo hivyo ambavyo havina maadili ya kazi za Polisi”
Aidha jalada tayari limefunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo, na kuomba wananchi watoe ushirikiano kutoa taarifa za wahusika ili kuwachukulia hatua watu au askari waliohusika na matukio hayo ya kuwapiga wananchi.
No comments:
Post a Comment