Katika maadhimidho hayo yaliyobeba kauli mbiu maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo yaliambatana na gwaride maalum LA kijeshi pamoja na kwaya mbali mbali kutoka shule ya weru weru,shule za sekondari kutoka Zanzibar pamoja na Dodoma wakihamasisha utunzaji wa mazingira ikiwa tunaelekea uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda.
Akizungumza katika maadhimisho hayo makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh samia suluhu hassan amesema umoja wa mataifa umekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania kwa kipindi kirefu huku akisisitiza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu unaendana vena kabisa na dira ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka2025 na ya awamu ya pili ya mpango wa taifa wa miaka mitano unaoanzia 2016/2017 hadi 2020/2021 unaokusudiwa kishajisha Tanzania kuingia katika uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025
.
Aidha makamu wa rais ametoa wito kwa timu ya viongozi ya umoja wa mataifa nchini kuunganisha mafanikio yaliyokwishapatikanika kupitia utekelezaji unaoendelea kutekelezwa.
Naye Mratibu mkazi wa umoja wa mataifa na mwakilishi mkazi wa UNDP bwana Alvaro Rodriguez amekazia mafanikio yaliyopatikana chini ya mpango wa kwanza wa umoja wa mataifa wa msaada wa maendeleo na vile vile utekelezaji wa mapema wa awamu ya pili ya mpango wa umoja wa mataifa wa msaada unaoweka mkazo katika malengo ya maendeleo endelevu na mipango ya maendeleo ya taifa kwa upande wa bara na Zanzibar.
Vile vile bwana Rodriguez amesema miradi ya umoja wa mataifa umekuwa ukilenga jamii wenyeuhitaji maalum wakiwemo watoto na wanawake pia akiangazia program kabambe ya pamoja ya kigoma ambayo hivi sasa inafadhiliwa na Norway na Koica ambayo imebuniwa maalum ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa wa kigoma na hasa kwa kuzilenga jamii za wenyeji wa Tanzania katika wilaya tatu za kasulu,kibondo na kakonko ambazo zinahifadhi zaidi ya wakimbizi 300,000
No comments:
Post a Comment