• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 24 October 2017

    Wizara ya afya ustawi wa jamii
    jinsia watoto na wazee imepokea vifaa kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya kizazi ikiwa ni mpango wa upanuaji wigo wa utoaji huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi. 
    Hayo yamezungumzwa Leo na waziri  ummy mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  wakati akiwakabidhi  msd vifaa hivyo kwa ajili ya usambazaji wa vifaa Tiba hivyo ambapo mh amesema kuwa wizara imepokea  mashine 100 aina ya trayothirup na mashine9 kwa ajili ya upasuaji mdogo pamoja na mitungi 179 ya gesi itakayowezesha mashine hizo kufanya kazi na gharama yake kufikia bilioni moja.
    Aidha mh ummy amesema ugonjwa wa saratani umekuwa tishio kubwa kwa nchi yetu kwani kwa mujibu wa takwimu ya taasisi ya saratani ya ocean road inaonyesha kuwa saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kwa 34%ikifuatiwa na saratani ya ngozi13%,saratani ya mfumo wa chakula10%,saratani ya kichwa na shingo7%,saratani ya matezi9%,saratani ya damu4%saratani ya kibofu ikiwa ni 4%.

    Hata hivyo mh ummy amesema 80% ya watu wanaofika hospitalini kutibiwa wanakuwa wamefikia katika hatua za mwisho hivyo watahakikisha wanakabiliana na tatzo hill kwani vituo vitoavyo huduma hivyo vimeongezeka kwani halo awali vilikuwa 343 lakini Sasa ni vituo443. Hivyo amewataka wanachi wrote kujitokeza kupima kwani huduma hizo ni katika zahanati zote,hospital za wilaya na hospitali za mkoa.
    Vile vile mh ummy amesema vifaa hivyo vitasambazwa katika mikoa ya Mara,singida,manyara,ruvuma,Lindi na mtwara vile vile amewataka wahudumu katika hospitali zote kuvitumia vizuri na kuvitunza vizuri.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI