• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 19 October 2017

    MAADHIMISHO YA SIKU YA UMOJA WA MATAIFA (UN) OKTOBA 24

    Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje Dakta Susamn Kolimba amesema oktoba 24 mwaka huu kutakuwa na maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa UN ambapokitaifa yatafanyika jijini  Dar es salaam katika viwanja vya ,karijee, mgeni rasmi atakuwa  Makamu wa raisi Samia Suluhu.

    Hata hivyo Dakta Kolimba amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na gwaride maalum pamoja na kupandishwa bendera ya umoja wa mataifa , wageni mbalimbali watakuwepo wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali ,vyombo vya usalama, wanafunzi  pamoja na wananchi.

    Kauli mbiu ya maadhimisho hayo itakuwa ''MAENDELEO YA VIWANDA YAZINGATIWE,UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA MAENDELEO ENDELEO''

    Kwa upande wa mwakilishi wa umoja wa mataifa Alvaro Rodrigez amesema wanaipongeza serikali ya Tanzania kuendelea kuleta maendeleo ya nchi ,uhifadhi wakimbizi wengi na wataendelea kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo nchini kwa ajili ya watanzania.
    Mwandishi Apolonia Kisite

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI