Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka
Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akisalimiana na
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA)
Kapteni George Simbakalia alipokuwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya
uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo.
Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka
Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi akitazama jiwe la
msingi la mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara yake
wilayani Bagamoyo leo. Waziri huyo ametembelea maeneo ya uwekezaji ya
Mamlaka ya Maeneo ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA), maeneo ya Kihistoria la
Kaole na eneo itakapojengwa bandari.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya akielezea jambo mbele ya Waziri
wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed
Al–Rumhi alipotembelea eneo la bandari ya Bagamoyo wakati wa ziara yake
kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani Bagamoyo leo. Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Naibu Waziri wa Utalii wa
Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi (mwenye ushungi).
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya akipokea zawadi toka kwa Waziri
wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi
wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji wilayani Bagamoyo leo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majjid Hemed.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo akiwaonyesha eneo la bahari ujumbe kutoka Serikali ya
Oman unaoopngozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi kutoka Serikali ya Oman
Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (mwenye miwani mwenyeusi) walipotembelea
eneo la Bandari ya Bagamoyo iliyopo Mbegani katika ziara ya kutembelea
maeneo ya uwekezaji na historia wilayani Bagamoyo leo. Mwenye vazi la
kitenge ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi
Stellah Manyanya.
Waziri wa Mafuta na Gesi
kutoka Serikali ya Oman Dkt. Mohamed Bin Hamed Al–Rumhi (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania
mara baada ya kutembelea eneo itakapojengwa bandari mpya wilayani
Bagamoyo leo. Kushoto ni Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. Al
Mahruqi, Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima, Naibu Waziri wa
Utalii wa Oman Bi. Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo,Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya, Waziri wa Uwekezaji wa Oman Salem
Bin Nasser Al Ismaily. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO
No comments:
Post a Comment