• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 19 October 2017

    WAIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU JUU YA WATAFITI WALIOPO KIJIJINI

    Image result for ndalichako

    Wakazi wa Kata ya Itololo wilayani Kondoa Wameitaka Serikali kuwapa Faida na Elimu Juu ya Utafiti unaotarajiwa kuanza kwenye Mapango yalipo kwenye kijiji cha Machinjioni  na kuwashirikisha wageni kutoka njee ya nchi bila kupewa elimu wala taarifa kutoka kwa viongozi wa wizara ya maliasili na utalii aua ofisi ya Mkuu wa wilaya.

    Akizungumza na wanahabari walitembelea kijijini Hapa Diwani Mstaafu Yahaya Giriki alisema kuwa zoezi la utafutaji wa malikale katika eneo hilo haujawashirikisha wananchi kwa kupewa elimu juu ya utafiti huo.

    Amesema kuwa suala hilo wao wameona wageni kutoka mataifa ya nje kufika na kuanza kuongea na wananchi na serikali ya kijiji na wageni kuahidi kuchangia ujenzi wa shule bila kuwashirikisha viongozi kutoka ngazi za juu ikiwemo ngazi ya wilaya na kufika nao kwetu kututambulisha.

    “Unajua Ndugu wanahabari Suala hili linatatiza sana hatujui faida ya utafiti huu na nini kinakuja kuvumbiliwa hapa tunaona mahema yamejengwa na wanasema kuna watu kutoka wizarani wamekuja nao lakini hapo awali walikuja wao kama wao bila hata mtu kutoka wizarani tutaamini vipi” alisema Giriki.

    Nae Mmoja wa wajumbe wa serikali ya kijiji hicho anasema kuwa wanatambua wageni hao kufika kijijini kwao miezi kadhaa iliyopita na kuzungumza na wajumbe wa kijiji na baadae kuongea na wananchi na kukubaliana kuwa wanakuja kuvumbua mifupa na mabaki ya dhana za kale kwenye eneo lililopo na kujulikana kama Kisese ii.

    Amesema kuwa waliafiki jambo hilo kwa faida ya wananchi na waliomba kupatiwa msaada wa ujenzi wa shule ya msingi ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi upauzi wa paa na umaliziaji wa madarasa mawili na wageni hao kukubali nakuanza ujenzi huo kama mnavyoona na wao wamefika hapa teyari kuanza utafiti wao.

    Suala la wageni kutoka nje ya nchi kwenda kufanya utafiti kwenye kijiji hicho cha Machinjiono limegubikwa na sintofahamu hadi mda huu kutowepo na barua yeyote kutoka eneo lolote ndani ya wilaya kwenda kwenye uongozi wa kijiji hicho licha ya kuonekana kwa mahema juhudi za kumpata kiongozi wa watafiti hao aliyetambuliwa kwa jina moja la Catherine Raia kutoka nje anayesoma chuo kikuu cha Dar es salaam.

    Hata hivyo juhudi zinaendelea kumtafuta Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii au Mkurugenzi wa malikale waweze kuelezea kama wanalijua suala hilo na hatua gani zimechukuliwa kuwapa taarifa wananchi kuhusu kadhia hiyo au suala hili lipo kinyume na sheria.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI