Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya
kufanya mazungumzo na ugeni kutoka Taasisi inayoshughulikia masuala ya
mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40 CITIES) ofisi kwake Karimjee,wa
kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings
Chikoko, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia
kutoka Jijini London Simon Hansen.
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES
Kanda ya Afrika Hastings Chikoko akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaa
Isaya Mwita ,kushoto Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote dunia
kutoka Jijini London Simon Hansen.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita katikati akiwa pamoja na ugeni kutoka Taasisi
inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia ya Nchini Dunia (C40
CITIES) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote
dunia kutoka Jijini London Simon Hansen, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES
kanda zote dunia kutoka Jijini London Simon Hansen akizungumza wandishi
wa habari leo mara baada ya kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji
la Dar es Salaam Isaya Mwita aliyesimama katikati, wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES Kanda ya Afrika Hastings Chikoko.
Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji.
……………
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Isaya Mwita, amesema mipango thabiti iko mbioni ili kuboresha
miundombinu yenye changamoto dhidi ya mafuriko na majanga mbalimbali
yanayoweza kulikumba jiji hilo.
Meya Mwita aliyasema hayo leo
alipokutana na kufanya mazungumzo na ugeni kutoka taasisi
inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi duniani (C40 CITIES)
ofisini kwake Karimjee jijini hapa.
Ugeni huo uliwakilishwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa C40 CITIES Kanda ya Afrika, Hastings Chikoko na
Mkurugenzi Mkuu wa C40 CITIES kanda zote duniani kutoka London,
Uingereza.
Amefafanua kuwa katika mazungumzo
hayo wamekubaliana kuleta mtalaamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi
ambaye atafanya kazi ya kushughulikia changamoto mbalimbali
zinazohusiana na masuala ya mabadiliko hayo jijini hapa.
Amesema pia wameahidi kutoa
fedha kwa ajili ya kuboresha maeneo ambayo yanakumbwa na mafuriko mara
kwa mara likiwemo bonde la Mto Msimbazi, Jangwani na maeneo mengine.
“Leo nimekutana na marafiki
zetu hawa wa C40 CITIES, tumeongea mambo mengi ya kujenga na kuliletea
jiji letu maendeleo katika sekta ya miundombinu ambayo imekuwa ni
changamoto katika jiji letu.
“Jiji letu linakua kwa kasi kubwa,
tunatakiwa kujipanga mapema, maeneo mengi yanakumbwa na mafuriko wakati
wa mvua, wananchi wetu wanahangaika, sasa imefika kipindi ambacho
tunapaswa kulipatia ufumbuzi jambo hili,” amesema Meya Mwita.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
C40 CITIES, Hastings Chikoko, amesema kuwa wamekuja jijini hapa kwa
ajili ya kusaidiana katika maeneo matatu ambayo ni usafiri jijini,
kukabili mafuriko na ukame ili kuwezesha kilimo cha mijini.
Alisema taasisi hiyo itatoa
mtaalamu/mshauri mmoja ambaye atafanya kazi kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa muda wa miaka mitatu ili kutoa
mapendekezo ya namna watakavyokabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi ili jiji liwe salama.
No comments:
Post a Comment