Afisa
Mipango wa kituo cha huduma za sheria tawi la Pemba Khalfan Amour
amewataka vijana nchini wawe na utamaduni wa kujifunza sheria za nchi
kwani kufanya hivyo kutawaongoza katika kufanya majumuku yao vizuri na
pia itakua dira ya maendeleo katika maisha yao.
Ameyasema
hayo leo huko katika ukumbi wa kituo cha huduma za sheria ZLSC upande
wa Pemba maeneo ya chakechake mjini alipokua akingumza na vijana wa
mkoa wa kusini Pemba katika kikao maalumu cha tathmini juu ya mafunzo
mbalimbali ya taratibu za uwandaaji wa katiba na sheria tofauti za nchi
kupitia mafunzo waliyowahi kuwapa vijana hao.
Khalfan
alisema , kutokana na mafunzo waliyowapatia vijana wa mikoa yote miwili
ya Pemba yameonysha mabadiliko makubwa kwao na hata jamii zao kwa
mujibu wa maelezo ya vijana wenyewe.
"hali
inaonekana tofauti, awali vijana hawa walikua hawana uwelewa wa sheria,
kama vile sheria ya mabaraza ya vijana , sheria nambaro 16 ,2013 ambayo
moja kwa moja sheria hii inahusiana na vijana wenyewe, wengine
waliingia katika mabaraza ya viajana ilhali hawajui lolote, lakini hivi
sasa inaonekana wamepata mwamko na uwelewa wa sheria mbalimbali" alisema
Khalfan
Mmoja
miongoni mwa washiriki katika kikao hicho , Mohd Khamis Suleiman
kutokea Mahuduthi Kengeja alisema, anakishukuru sana kituo cha huduma
za sheria Pemba kwa msaada wao wa kuwajuza masuala ya kisheria kwani
hivi sasa amepata kujua sheria mbalimbali za nchi pamoja na kuijua
katiba yake inayoongoza nchini.
Alisema
, mara baada ya kupata taaluma hiyo aliamua kwenda kijijini kwake
kuwafikishia vijana wengine taaluma hiyo , ingawa alipata changamoto
kadhaa zilizokua zikimkwaza ikiwamo suala zima la siasa lakini
hakukubali kuyumba na angali anaendelea kutoa taaluma hiyo na wanachi
wanaindelea kukubali.
Alisema
changamoyo anazokabilaiana nazo , wananchi wengi wao wanachanganya
mambo ya sheria na siasa "unapokwenda kuwaelekeza vijana ili wawe na
mwamko katika sheria, wanasema nyinyi ni CCM tu , kidogo inarejesha
nyuma" alisema Suleiman.
Zuwena
Nassor Salim kutoka chambani, kwa upande wake alisema , amefurahishwa
na utaratibu wa kituo cha ZLSC kuwajali vijana kwa kuwapatia taaluma
hiyo ya kisheria kwani pia imemsaidia kujua sheria za nchi katika katiba
pamoja na kuelewa umuhimu wa vijana kujiunga na mabaraza ya vijana.
Kupitia
uwelewa wa kisheria aliyoupata kutoka ZLSC Salim alisema, aliamua
kwenda kushajihisha vijana na wezee katika kijiji chake ili waone
umuhimu wa vijana kujiunga na mabaraza hayo na alichokigundua ni kuwa,
bado wananchi wana uwelewa mdogo wa sheria kwani wengi miongoni mwao
wanaamini mabaraza ya vijana ni maalumu kwa watu wasiokua na heshima
" ukiwashajihisha wajiunge katika baraza la vijana wanasema ni mabaraza ya watovu wa adabu" alisema Salim.
Aidha
aliendelea kusema kuwa, kuna baadhi ya wananchi kijijini kwao
wanaitikadi kuwa kujiunga na mabaraza ya vijana ni kuisadia CCM kura za
ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2020 jambo ambalo alipinga na kusema si
kweli bali mabaraza ya vijana ni maalum kwa lengo la kuwatafutia njia
mbadala vijana ya kufikia maendeleo katika maisha yao.
Katika
hatua nyengine alisema , ingawa changamoto hizo zipo lakini anaendelea
kupambana nazo na hali inaonekana kubadilika na wengi miongoni mwa
wananchi wanaonekana kuwa waelewa.
Kwa
Upande wake mwanafunzi kutoka katika skuli ya Connecting Continental
Secondry School ambae pia aliwahi kupokea mafunzo ya sheria kupitia ZLSC
Pemba Intisar Ahmed Saleh alisema kutokana na uwelewa wa sheria
aliyonao, linapotokeza tatizo la kisheria kwa upande wake anajua wapo
pakuelekea.
Alisema,
watu vijijini na wananchi kwa ujumla wengi wao hawana uwelewa wa
kutosha katika mambo ya kisheria hivyo kwa makusudi aliamua kuwaita
wanafaunzi wenzake na kuanza kuwashajihisha kupenda kujua sheria pamoja
na kuwafundisha kile alichokipata kutoka katika kituo hicho na kwa
kiwango kikubwa wamekubaliana na uwamuzi huo.
Kituo
cha huduma za sheria ZLSC upande wa Pemba kimekua kikishuhudiwa kutoa
mafunzo ya kesheria ikiwamo haki za binaadamu, katika na nyenginezo kwa
kada tofauti kama vile askari , walimu, wanafunzi, masheha na mashehe,
vijana na wengineyo.
No comments:
Post a Comment