• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 8 October 2017

    Mike Pence aondoka uwanjani baada ya wachezaji kupinga ubaguzi

    Mike Pence tweeted a photo of himself standing during the US national anthem at an NFL game on Sunday, 8 October 2017
    Aliondika baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa

     
    Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, ameondoka kutoka kwa mechi ya kandanda ya NFL nchini Marekani, baada wachezaji kukataa kusimama wakati wa kuchezwa kwa wimbo wa taifa wa Marekani.
    Bw. Pence alisema kuwa hatakuwa kwenye warsha ambayo haiheshimu wanajeshi wa Marekani au bendera baada ya kuondoka kwenye mechi iliyokuwa ikichezwa katika jimbo nyumbani kwake huko Indiana.
    Rais Donald Trump aliandika katika mtandao wa twitter kuwa alimuomba Pence kuondoka ikiwa wachezaji wangepiga magoti.
    Kupiga magoti wakati wa mechi za NFL imekuwa njia ya kupinga ubaguzi wa rangi

    Mike Pence aliondika baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa
    Trump amewakosoa wachezaji vikali na kuitaka NFL kuwapiga marufuku.
    "Niliondoka katika mechi ya leo kwa sababu rais Trump na mimi hatutakubali warsha yoyote ambayo haieshimu wanajeshi wetu, bendera yetu au wimbo wetu wa taifa," Pence aliandika kwenye twitter siku ya Jumapili.
    US Vice-President Mike Pence and President Donald Trump during the US national anthem
    Aliondoka baada ya wachezaji wa timu ya San Francisco 49ers haikusimama wakati wa wimbo wa taifa kabla ya mechi dhidi ya Indianapolis Colts.
    Awali Bw. Trump alisema kuwa matamshi yake ya kukosoa hatua za NFL hayakuhusu kwa vyoyote vile suala la rangi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI