Mwakilishi wa kundi la Vijana
Group Bw.Timotheo Umbayda (kulia) akieleza jambo kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu utafiti kwa vijana pamoja na utendaji
kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katika ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari Idara ya habari
–MAELEZO Bw.Frank Shija .
Picha na Paschal Dotto-MAELEZO
…………….
Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Muungano wa vijana kutoka Karatu
mkoani Arusha maarufu kama Vijana Group wamemuomba Rais Mh.John Pombe
Magufuli kudhibiti vijiwe vya Pombe na Kamari vinavyopotezea muda vijana
ili wajikite katika shughuli za ujenzi wa wa taifa kama sera ya
serikali ya wamu ya tano ya Tanzania ya viwanda inavyoelekeza.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es
Salaam jana na Bw.Timotheo Umbayda alipozungumza na waandishi wa habari
juu ya utafiti kuhusu vijana na ujenzi wa taifa utafiti iliofanyika
katika mikoa 8 ya Tanzania bara yakiwemo Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza
na Arusha huku utafiti huo ukijikita zaidi kuchukua maoni ya vijana juu
ya utendaji kazi wa serikali ya Awamu ya tano pamoja na changamoto
zinazowakabili vijana katika mikoa hiyo.
“Wakati umefika Mh.Rais aone namna
ya kuwasaidia vijana wanaoshinda kwenye vijiwe vya Pombe, na wale
wanaoshinda kwenye michezo ya kubahatisha na pool table, waondokane na
tabia hizo na hatimaye wafanye kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi
na ya taifa kwa ujumla”,alisema Bw.Umbayda
Aidha Bw.Umbayda alisema kuwa
katika utafiti wao wamebaini kuwa vijana wengi wa kitanzania hasa
waishio mijini wamekuwa wakiutumia muda wao vibaya hususan kufanya maovu
badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo na uzalishaji
mali.
Alisema vijana ndio kioo cha jamii
hivyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taifa linapata
maendeleo, hivyo wakijielekeza katika kukaa vijiweni kusikokuwa na tina
Tanzania haitaweza kupata maendeleo na itaendelea kuwa tegemezi wakati
nguvukazi ya kutosha ipo na ina uwezo wa kufanya kazi.
Aliendelea kusema kuwa Rais
Magufuli atoe maelekezo kwa vijana kupitia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na
wakuu wa Wilaya ya jinsi ya kuwasaidia vijana ili washiriki katika
kujenga uchumi kwa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali, ufundi,
ufugaji na ujasiriamali ili kuongeza nguvu katika ukuaji wa uchumi.
Bw. Umbayda alisema kuwa katika
kuwajenga vijana kimaadili ni muhimu kwa taifa kuwashirikisha viongozi
wa dini katika kuwaombea na kuwafundisha maadili kwani taifa lenye
maadili ndiyo taifa lenye maendeleo.
Kikundi cha Vijana group kinaundwa
na vijana watano wa kitanzania kutoka Karatu mkoani Arusha, ambao ni
waalimu na lengo la kikundi chao ni kutumia taaluma yao ya ualimu
kufundisha vijana jinsi ya kutumia vizuri muda na kujiletea maendeleo
badala ya kukaa vijiweni.
Hivi karibuni vijana wengi hasa wa
mijini wameingia kwenye wimbi la kukaa vijiweni bila kufanya kazi
yoyote huku wakishiriki katika michezo ya kubahatisha maarufu kama
‘Kubeti’ badala ya kufanya kazi
No comments:
Post a Comment