Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Andrew Mwalwisi akizindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya JKCI Prof. William
Mahalu na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed
Janabi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la
Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Restituta Rugaganya mara baada ya kuzindua baraza
hilo leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed
Janabi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Andrew Mwalwisi akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa baraza la
Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Rajabu Matiku mara baada ya kuzindua baraza hilo
leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed
Janabi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Andrew Mwalwisi akimpongeza Katibu wa baraza la Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Samweli Rweyemamu mara baada ya kumkabidhi vitendea kazi
wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
William Mahalu akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa
Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa
baraza uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu mwenyekiti
wa TUGHE Rajabu Hamisi.
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya tawi la Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Msaidizi
wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Ulemavu
Andrew Mwalwisi wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi
la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Mkutano
wa kuzindua baraza la Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi
la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ukiendelea.
Picha na JKCI
…………..
WAJUMBE
WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE WATAKIWA
KULITUMIA BARAZA HILO KUFIKISHA MALALAMIKO YAO NA KUTOA MAONI NA SIYO
VINGINEVYO
Na Mwandishi wetu
11/10/2017
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa
kulitumia Baraza la wafanyakazi kufikisha malalamiko yao na kutoa maoni
ya utendaji kazi na siyo vinginevyo.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Andrew Mwalwisi wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) tawi la JKCI.
Alisema
baraza hilo ni la muhimu kwani ndilo linalotambulika kwa mujibu wa
kisheria kama watalitumia vema kufikisha malalamiko yao, maoni na
ushauri wa sheria na si kulitumia kama ‘forum’ (majukwaa) ambayo
hayatambuliki kisheria litawasaidia kuimarisha mahusiano mazuri baina ya
viongozi na wafanyakazi.
“Ninaimani
kubwa kwa uongozi wa taasisi hii kwamba utapokea malalamiko, ushauri
na maoni ya wafanyakazi wake kupitia baraza hili na kuyafanyia kazi.
Hatua hiyo itasaidia kuboresha utendaji kazi wa taasisi hii katika
kuhudumia wagonjwa (wateja)”, Mwalwisi alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema
kuzinduliwa kwa baraza hilo kunadhihirisha jinsi ambavyo taasisi hiyo
imekua katika utoaji huduma.
“Kwa
hiyo leo kwetu ni siku muhimu kwani baraza hili lililozinduliwa ni la
muhimu litatusaidia katika kuimarisha utendaji kazi wa taasisi,”
alisema.
Prof.
Janabi aliwasisitiza wajumbe waliochaguliwa kuliongoza baraza hilo kuwa
chachu katika kutimiza wajibu wao kuisaidia taasisi kuendelea kutimiza
dhima yake ya kutoa huduma bora za kimatibabu na za kitafiti ili iweze
kufikia lengo iliyojiwekea la kuwa kituo bora cha kutoa huduma za afya
ya moyo Afrika.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi hiyo Prof. William Mahalu
aliupogeza uongozi wa Taasisi kwa kusimamia na kuhakikisha Baraza la
wafanyakazi linaundwa na kuanza kufanya kazi zake kwa wakati.
Prof.
Mahalu alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo huu ni mwaka mmoja na
nusu wameweza kuwa na baraza la wafanyakazi jambo ambalo siyo rahisi
kwani wengine wanakaa hadi miaka mitatu wakibisahana nani awe Katibu wa
kuliongoza baraza lao.
No comments:
Post a Comment