Akizungumza ofisini kwake leo Jumatatu, Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema tukio hilo lilitokea jana
Jumapili saa 10:00 jioni nyumbani kwa mganga huyo, alipokuwa anamuwekea
dawa ya unga kupitia tundu la uume wake kisha kuanza kuisukuma kwa
kutumia pampu ya kujaza upepo kwenye baiskeli.
Kamanda Haule amesema wakati akipampu ili dawa hiyo iingie
vizuri ndani, mzee huyo alianza kutokwa damu nyingi kwenye tundu hilo na
kisha kuishiwa nguvu.
“Kutokana na kutokwa damu nyingi ilisababisha kifo cha mzee
huyo, ambapo tayari jeshi la polisi linamshikilia mganga huyo kwa tuhuma
za kusababisha kifo cha mzee Joseph,” amesema Kamanda Haule
Amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda Haule aliwataka wananchi
kuacha kuona waganga kuwa kimbilio la matatizo yao badala yake wakimbile
hospitalini au kwenye vituo vya afya vilivyokaribu nao.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment