Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum
Hapi ametoa siku saba kwa muwekezaji anaemiliki mgahawa wa Tangren
uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa
mgahawa huo wanalipwa stahiki zao za malimbikizo ya muda mrefu.
Akizuungumza jijini Dar es Salaam
alipotembelea mgahawa huo DC Hapi baada kupokea malalamiko kwa
wafanyakazi wa mgahawa huo ambao wamedai kutolipwa malimbikizo yao kwa
muda miaka kumi, na wamekuwa wakifanya kazi bila likizo wala 'over
time', DC Hapi ameagiza stahiki zao zishughulikiwe ndani ya siku saba.
Pia DC Hapi ameagiza wafanyakazi hao
waunganishwe kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii haraka iwezekanavyo na
wapewe mafunzo ya namna inavyofanya kazi.
" Tunapenda sana wawekezaji lakini sio
wawekezaji wasiofuata misingi na taratibu na sheria za nchi, namuomba
muwekezaji huyu azingatie maagizo niliyotoa vinginevyo tutachukua hatua
zaidi" Alsema DC Hapi.
DC Hapi ameeleza kuwa watafanya
oparesheni ya kuwafutia leseni za biashara na kuwachukulia hatua
wawekezaji wasiofuata sheria na taratibu za nchi, ambapo amesisitiza
kuwa haitaji wafikie huko endapo watafuata sheria.
Katika hatua nyingine DC Hapi amewataka
wafanyakazi kuwa na nidhamu ya kazi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha
kutoa visingizio visivyokuwa na sababu ya msingi kama walivyo
lalamikiwa na mmiliki wa mgahawa huo Liu Deng Wei ambaye ameeleza kuwa wafanyakazi hao wamekuwa wakichelewa kufika kazini na kutoa visingizio visivyokuwa na msingi.

Pia DC Hapi katika ziara yake alitembelea kiwanda cha kutengeneza lifti cha SEC East African kilichopo Masaki na kuutaka uongozi wa kampuni hiyo kuweka mahusiano mazuri na wafanyakazi wao ili kutatua changamoto zinazowakabili.
DC Hapi amewashutumu vikali baadhi ya
viongozi kutoka Wizara ya Kazi wanaoshirikiana na muwekezaji kuwanyonya
watanzania wanyonge na kuhaidi atazifikisha taarifa kwa mamlaka ya juu
wazifanyie kazi.






No comments:
Post a Comment