Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa watendaji wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wakati alipotembelea Ofisi za Wizara zilizopo UDOM Dodoma.
………………..
Na Kitengo cha Mawasilia WAMJW
Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndungulile amewataka watendaji wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuwa na mkakati wa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika kazi za maendeleo yao.
Mhe. Dkt. Ndungulile ametoa kauli hiyo mjini Dodoma alipotembelea katika Ofisi ya Wizara yake iliyoko Chuo Kikuu cha Dodoma na kuzungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mhe. Dkt Ndugulile ameshauri Wizara kuendeleza jukumu lake walilolianza la kuhamasisha jamii kuchangia kazi za maendeleo ili kupunguza kiwango cha utegemezi katika kutatua changamoto zilizopo.
“Niwapongeze kwa juhudi mnazozionesha za kuhamasisha wananchi kufanya kazi za kujiletea maendeleo” alisema Mhe. Dkt Ndugulile
Aidha Mhe. Dkt Ndungulile amempongeza Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga kutokana na utendaji kazi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto.
Naibu Waziri pia amehimiza Wizara kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa kwa wazee na watoto walioko katika mazingira hatarishi, ili kuweka mazingira salama na rafiki kwa wazee na watoto wote wanaohitaji huduma maalum.
Kwa upande wake Katibu Mkuu IdaraKuu Maendeleo ya jamii, Jinisa, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amepongeza Naibu Waziri Dkt Ndugulile na kumhakikishia ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya Wizara.
Naibu Waziri Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile ametembelea Ofizi za Wizara zilizopo Makao Mkuu Dodoma ikiwa ni siku chache tangu kuapishwa kushika wadhifa huo.
No comments:
Post a Comment