Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu nane wamefariki dunia na zaidi ya watu kumi na wawili wamejeruhiwa na gari iliyopamia waendesha basikeli mjini humo.
Bill amelielezea tukio hilo ni ugaidi wa namna yake kwa umati wa watu kupaamiwa na kuzua hofu mjini humo.
Kamishna wa polisi wa jiji la New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyehusika kutekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka ishirini na tisa aliyekuwa anaendesha gari aina ya gari ndogo ya kubebea mizigo aliyokuwa ameikodi.
Alisema gari hilo liliwagonga waenda kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.
Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka kwenye lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya utekelezaji polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii.
Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Manhattan ya chini.
Vyombo vya habari nchini Marekani wamenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Manhattan ya chini ,kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga
No comments:
Post a Comment