Naibu Waziri Wa Afya Mheshimiwa Faustine Ndugulile (Mb) leo
amemuwakilisha Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu katika uzinduzi wa Kampeni Ya Upimaji
Macho, Shinikizo La Damu Na Kisukari Mkoani Pwani katika Wilayani
Mkuranga.
Katika hatua hiyo Naibu Waziri Amempongeza Mwenyekiti Wa
Lions Club kwa jitihada anazofanya za kuunga mkono juhudi za Serikali Ya
Awamu Ya Tano kwa kampeni anayoendelea nayo ya huduma ya upimaji wa
afya bure katika jamii.
Aidha, Naibu Waziri Wa Afya ameeleza utafiti uliofanywa na
Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na Shirika La Afya Duniani (WHO) na Taasisi Ya NIMR wa
Mwaka 2013, unaohusu Viashiria Vya Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukiza,
umeonyesha Kuongezeka kwa viashiria hivyo, idadi ya Watanzania wenye
shinikizo la damu ni asilimia 25.9% na wagonjwa wa kisukari ni asilimia
9.1%.
"Hii Haikubaliki, ni lazima tuongeze bidii katika
kuyashughulikia magonjwa haya. Ni lazima Kwa pamoja Serikali Na Sekta
Binafsi tufanye kazi kwa bidii katika kupambana na janga hili ambalo
visababishi vyake vikubwa ni pamoja na ulaji usiofaa, kutokufanya
mazoezi, matumizi ya pombe na tumbaku kupita kiasi " alisema Dkt
Ndugulile
Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Serikali inafanya kazi kwa
kushirikiana na Wadau katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya
kujikinga na maradhi yasiyo ya kuambukiza kupitia njia mbalimbali.
Katika hatua hiyo kliniki zipatazo 187 za magonjwa yasiyo
ya kuambukiza zimeanzishwa na kuimarishwa, kuanzia ngazi Ya Vituo Vya
Afya mpaka Hospitali Ya Taifa.
Aidha, Mheshimiwa Naibu Waziri alipata fursa ya kutembea
kiwanda cha KNAUF ambacho kinajishughulisha na uzalishaji wa Gypsum
Board Na Gypsum Plaster Na kuwapongeza kwa juhudi wanazofanya za kuunga
mkono Sera Ya Viwanda Nchini
Naibu Waziri aliwashukuru Uongozi mzima wa Lions
Club Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Madaktari wa hospitali ya Regency
na Wilaya ya Mkuranga kwa kumualika na kuahidi Serikali Ya Awamu Ya
Tano itaendelea kuunga mkono juhudi zote wanazofanya na kuahidi kuwapa
ushirikiano wa karibu pindi watapohitaji.

No comments:
Post a Comment