• ..

    ..

    Friday, 27 October 2017

    Matembezi ya hisani kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti.

    Image result for ocean road tzTaasisi ya ocean road kwa kushirikiana na hospital ya Aghakhan imeeandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika kesho kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani pamoja na kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wa saratani.

    Hayo yamezungumzwa Leo na mkurugenzi mtendaji wa taasisi yasaratani ocean road bwana mwakasegele alipokuwa akizungumza na waandishi habari kuhusiana na matembezi hayo yataambatana na uchangiaji damu kwaajili ya wagonjwa wa saratani.

    Aidha mwakasegele amesema kuwa taasisi ya saratani ya ocean road imeshapiga hatua kubwa ktk kutekeleza majukumu yake ikiwa pamoja na kuzuia saratani kwa kutoa elimu,kufanya uchunguzi wa saratani ili kugundua ikiwa katika hatua za awali na kutoa mafunzo ya hali ya juu ya saratani katika vituo mbali mbali nchini pamoja na kutoa matibabu ya tiba shufaa. Na sahihi kwa wagonjwa wa saratani na kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi kwaajili ya utafiti wa wagonjwa wasaratani .

    Hata hivyo bw.Mwakasegele amesema takwim inaonyesha katika mwaka 2016/2017 taasisi ya saratani ya ocean road ilihudumia wagonjwa27,900 wakiwemo wagonjwa wapya wa saratani 63,338,na wale wa marudio21,569 pia kati ya hao1,123 walikutwa na dalili za awali za matiti na shingo ya kizazi vilevile taasisi ilifanya uchunguzi wa saratani ya tezi dime kwa wanaume534 kati ya hao 227 walikutwa na dalili za awali za saratani ambapo kwa takwimu hizo inaonyesha wagonjwa wanaohudumiwa katika taasisi hiyo wanaongezeka.

    Nae mkurugenzi mtendaji wa Ocean road upande wa aghakhan bi.Lucy hwai amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika matembezi hayo ya hisani na kupima pia vile vile amewataka watanzania kujijengea dhana ya kupima  Mara kwa mara ili kujua maendeleo ya afya zao.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI