• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 25 October 2017

    Rais Magufuli apewa pongezi

       
    Image result for Dc mjemawafanyabiashara ndogondogo wa manispaa ya ilala maarufu kama machinga pamoja na madereva wa bodaboda wametoa pongezi kwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa jitihada mbalimbali anazofanya kuwapigania wanyonge na masikini nchini.

    pongezi hizo zilitolewa na shirikisho la umoja wa wafanyabiashara hao leo zilizotolewa katika uwanja wa shujaa ambapo mwenyekiti wa wafanyabiashara hao amesema mh.Magufuli anastaili pongezi hizo kwani amekua akitetea maslahi ya nchi pamoja na wanyonge kwani ameweza kupigania haki yetu watanzania kutoka katika kesi ya makenikia hadi tukaweza kupata bilioni 700 ambazo zisingepatikana bila jitihada zake na moyo wake wa ujasiri kwani watu wengi walikuwa wanamvunja moyo.

    hata hivyo mwenyekiti huyo wa shirikisho la wamachinga amemtaka rais asife moyo kwani shirikisho hilo lipo nyuma yake na linaunga mkono jitihada zake anazozifanya

    kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa madereva wa manispaa ya ilala bwana Athanasi Kitime amesema wanampongeza magufuli kwa kazi mbali mbali anazofanya huku akieleza kuwa changamoto mbalimbali wanazopata ni kutoruhusiwa kwenda katikati ya mji hivyo anaomba wapewe fursa hiyo ili waweze kwenda kupeleka na kufata abiria.

    naye mkuu wa wilaya ya ilala bi.Sophia mjema amesema anawashukuru wamachinga hao kwa kutoa pongezi kwa rais Magufuli kwani wao wametambua kazi anazozifanya magufuli na amesema kuwa watashirikiana na machinga hao bega kwa bega pia amewataka wamachinga hao waendelee kumuamini mh.Magufuli kwani ndoto zake ni za kweli na akiahidi kitu anatimiza.
    Image result for kairuki
    pia mh. Angela Kairuki ambae alikuwa mgeni rasmi katika pongezi hizo amesema atazifikisha pongezi hizo  rais pamoja na  risala alizokabidhiwa na viongozi wa shirikisho hilo na anaamini atazifanyia kazi huku naye akiungana na wafanyabiashara hao kumpa pongezi kwa kuzipigania bilioni 700 ambazo zimepatikana kupitia sakata la makinikia ambazo ni fedha nyingi kwa kuendeshea miradi mbali mbali.

    naye mbunge wa jimbo la ilala mh.Iddi zungu amesema amewapongeza wafanyabiashara wa manispaa hiyo kwa kutoa pongezi kwa raisi kwani pongezi za mnyonge ni baraka hivyo amemtaka mh.Magufuli atembelee kaliakoo kwa wafanyabiashara hao ajionee namna ambavyo wanaendesha shughuli zao na kuona changamoto mbali mbali wanazokutana nazo wafanyabiashara hao pia amewataka wafanyabiashara hao waishi katika umoja ambao utawaletea faida ili wawezekufungua akaunti yao ya benki ili waweze kukopesheka na kununua bidhaa zao wenyewe kwaumoja wao.

    katika pongezi hizo zilizoambatana na burudani ya muziki kutoka kwa msanii wa mziki wa singeli shollo mwamba ambae amekonga nyoyo kwa nyimbo zake mbali mbali.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI