Taarifa ambazo TFF imezipata
zinasema waliofariki dunia siku hiyo ni aliyekuwa Mchezaji wa timu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’; Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’; pamoja na
Afrika Mashariki miaka ya 1950 na 1960, Abdul Majham na Mwamuzi wa
Daraja la Kwanza anayechezesha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
Mirambo Tshikungu.
“Hakika nimepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za vifo hivi. Ni mshtuko mkubwa sana katika familia ya
mpira wa miguu hapa Tanzania, natambua pia ni majonzi makubwa kwa
familia za marehemu,” amesema Rais Karia.
“Niombe tu kwa familia, ndugu,
jamaa, marafiki, majirani kuwa watulivu katika kipindi hiki cha msiba.
Wawe na moyo wa subira baada ya ndugu zetu kutanguliwa mbele ya haki.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema, basi na tumuombe awe na
msamaha kwa ndugu zetu,” amesema.
Abdul Majham aliyefariki dunia
huko Visiwani Zanzibar ni Mchezaji huyo wa zamani wa Klabu ya Vikokotoni
ya visiwani Zanzibar, pia aliyepata kuichezea klabu Bingwa ya kwanza
ya Tanzania, Cosmopolitan ya Dar es Salaam.
Kuhusu Tshikungu, TFF imepokea
taarifa inayosema kwamba alifariki dunia jioni ya Oktoba, 2017 katika
Hospitali ya Ikonda iliyoko Wilaya ya Makete mkoani Njombe alikokuwa
akitibiwa.
Mwenendo wa uchezeshaji wake
ulikuwa na tija kwani rekodi zinaonesha kwamba mchezo wake mkubwa
kuuchezesha msimu uliopita ulikuwa ni kati ya Majimaji ya Songea na
Young Africans ya Dar es Salaam uliofanyika Uwanja wa Majimaji mkoani
Ruvuma.
……………………………………………………………………..……………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment